Shirika la Habari la Hawza | Usimamizi wa michezo ya kwenye simu kwa watoto unawezekana kwa kuweka mipaka kwenye muda, kuchagua michezo inayofaa, kupendekeza shughuli mbadala, na kuwa kielelezo kizuri kwa upande wa wazazi.
Tunawezaje kumwelewesha mtoto wetu kuhusu matumizi sahihi ya michezo ya kwenye simu?
Ili kuwasaidia watoto kutumia michezo kwa njia sahihi, unaweza kutumia mbinu zifuatazo:
1. Kuainisha muda maalum
- Weka muda wa kucheza kwa uwazi na kwa kuzingatia umri wa mtoto
(kwa mfano: lisaa 1 hadi 2 kwa siku).
- Tumia vifaa vya udhibiti kama kipima muda au programu za usimamizi wa matumizi.
- Baada ya muda uliowekwa kuisha, pendekeza shughuli mbadala kama vile kufanya mazoezi au kujisomea.
2. Kuchagua Michezo Inayofaa
- Chagua michezo kulingana na viwango vya umri (kama vile PEGI au ESRB).
- Tumia michezo inayo fundisha au ile inayohimiza ushirikiano, inayosaidia kukuza ujuzi wa kutatua matatizo au kufanya kazi kwa pamoja.
- Kagua maudhui ya mchezo kabla ya kuununua.
3. Kufanya mazungumzo kwa pamoja
- Zungumza na mtoto kuhusu madhara ya michezo ya mda mrefu (kutokufanya mazoezi, matatizo ya usingizi, kushuka kwa ufaulu shuleni).
- Tumia lugha rahisi na mifano ya maisha halisi (mfano: “Ukicheza sana, macho yako yatachoka”).
-Patiliza wasiwasi alio kuwa nao mtoto na mshirikishe katika kufanya maamuzi.
4. Kuhamasisha uadilifu
-Baadhi ya michezo ya kwenye kupyuta ifahamishe kwake kama sehemu tu ya ratiba ya kila siku.
-Himiza shughuli mbadala kama kuchora, kufanya mazoezi au michezo ya viungo.
- Panga muda wa kufanya shughuli za kifamilia, kama kutembea au michezo ya pamoja.
5. Kutumia vifaa vya uangalizi
- Wazazi wanatakiwa kuwapangalia muda (Parental Controls) kwenye michezo ya kompyuta ili kuzuia upatikanaji wa michezo isiyofaa.
- Kagua historia ya matumizi ya mtoto na toa mrejesho inapobidi.
6. Kuhamasisha uwajibikaji
- Mfundishe mtoto kwamba kudhibiti muda ni sehemu ya ukuaji wa tabia na utu.
- Ikiwa atafuata kanuni, mhamasishe kwa kumpa zawadi ndogo.
- Ikiwa hakufuata mipaka uliyo muekea, fuata hatua za kimantiki (kama kumpunguzia muda wa kucheza kwa siku inayofuata).
7. Kushiriki Pamoja na Mtoto kwenye mchezo
- Wakati mwengine cheza pamoja na mtoto ili kuimarisha mawasiliano na kuelewa maudhui ya michezo.
- Wakati wa kucheza, zungumza kuhusu maamuzi sahihi na yasiyo sahihi ndani ya mchezo (kama umuhimu wa kushirikiana au kuepuka vurugu).
8. Kumrejea mtaalamu ikiwa inahitajika
- Ikiwa mtoto anaonyesha dalili za ulevi kwenye michezo au tabia za ukatili, tafuta msaada kutoka kwa mwanasaikolojia wa watoto.
Maoni yako