Kwa mujibu wa ripoti ya kikundi cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, taasis ya ulamaa wa Yemen ilisema katika taarifa yake: "Katika kukabiliana na kuvunjwa kwa makubaliano na adui Muisraeli kutokana na uvunjwaji wa masharti ya mkataba, kuanza tena vita vya uharibifu na kutekeleza mauaji ya kimbari, ulamaa wa Yemen wamesisitiza kwamba hakuna udhuru kwa yeyote mbele za Mwenyezi Mungu na hakuna udhuru kwa wale waliozembea mbele ya Mwenyezi Mungu, na kwa watu wasiojali mbele ya Mungu hakuna msingi wa kuhalalisha."
Taasisi hii imesema pia: "Msimamo wa kulaani na kutaja maovu yaliyotokea na yanayoendelea kutokea Ghaza, na Palestina kutokana na vita vya uharibifu kwa mashambulizi ya makombora, au njaa, au kiu, mbele ya Mwenyezi Mungu haukubaliki."
Maoni yako