Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Abid al-Husayni, mmoja wa maulamaa mashuhuri wa Kishia nchini Pakistan, katika taarifa yake kuhusu vita ya hivi karibuni baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na utawala wa Kizayuni, ameieleza hali hiyo kuwa ni mapambano yaliyo zaidi ya mipaka ya kisiasa na kijeshi, na akaifasiri kuwa ni makabiliano kati ya kambi ya imani na kambi ya ukafiri.
Akiashiria uungaji mkono wa wazi wa Marekani, nchi za Ulaya na madola ya kibeberu kwa utawala wa Kizayuni, alisema wazi: Vita hii haikuwa tu kupambana na Israel, bali kwa hakika, nyuma ya utawala wa Kizayuni, kambi yote ya ukafiri wa kimataifa ilikuwa imesimama.
Maoni yako