Kwa mujibu wa habari kutoka Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Makarem Shirazi aliithamini siku ya ujenzi wa Msikiti wa Jamkaran.
Ujumbe wake ni kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezimungu mwingi wa rehma mwenye kurehemu.
Yanipasa kuanza mazungumzo haya hali ya kuwa ni mwenye kutarajia kwamba ibada zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani zitakubaliwa, na pia kutoa pole kwa kipindi hiki cha masiku ya kupata shahada Hadhrat Amirul-Mu’minin Ali (as).
Aidha, napenda kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Msikiti Mtukufu wa Jamkaran na kutakieni ninyi wote, pamoja na wahudumu wa Imam wa zama (a.s) na watu wa Iran kwa ujumla mwaka wenye baraka, ushindi, heshima, na afya kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Hii ni sehemu yenye nuru na ni ya kiroho, kama walivyosema watu wakubwa akiwemo Sheikh Saduq (r.a) amesema; msikiti hu umejengwa kwa amri ya wazi ya hadhrat Imam wa zama (a.s) mwenyewe, na wala si kwa ndoto bali ni kwa uongozi wa Hassan bin Muthla.
Zaidi ya miaka elfu moja, mahali hapa imekuwa ni sehemu ya siri na maombi ya karibu na Mwenyezi Mungu na kumkumbuka Mola wetu pamoja Imam wetu (a.s), na matendo ambayo yanahusiwa katika msikiti huu ni ya kipekee na yanasaidia katika kukuza roho na nafsi za waumini.
Picha za unyenyekevu na ibada za waumini, hasa vijana mbee za Mwenyezi Mungu na kutawasali kwa Imam (as) katika sehemu hii, zinakumbusha dua za waumini katika viwanja vya Arafat, kila mtu anayekuja hapa huja akiwa na huzuni pamoja na haja mbalimbali lakini anarudi akiwa na furaha pamoja na roho yenye uchangamfu hali yakuwa mikono yake imejaa majibu ya maombi yake.
Ni muhimu kwa waumini wote na viongozi muhimu kuhakikisha kuwa msikiti huu unaheshimiwa kwa hali yeyote inayo wezekana ili kuwavutia na kuhamasisha mioyo kuelekea sehemu hii tukufu, na kuhakikisha urahisi wa watu kufika na kufanya ziara kwa amani, inshaallah hili liwe ni lenye kuridhiwa na Hadhrat Imam (a.s).
Mwisho, natoa shukrani za dhati kwa nyote mliokusanyika hapa na hasa kwa msimamizi wa Msikiti wa Jamkaran, Hujjatul-Islam na Muslimin, Bwana Ajagh Nejad, na namtakia mafanikio tele Katika masiku haya na usiku wake, kwa unyenyekevu nakuomba kwa Mwenyezi Mungu ufanye haraka kudhihir kwa Imam wa zama (as).
Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullahi
Maoni yako