Kwa mujibu wa habari kutoka Shirika la Habari la Hauza, Ayatollah Nouri Hamedani katika ujumbe wake aliithamini siku ya ujenzi kwa Msikiti wa Jamkaran.
Ujumbe wake ulikuwa kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezimu mwingi wa Rehema mwenye kurehemu.
Ninamshukuru mwenyezimu bwana wa viumbe, na rehma na amani zimuendee bwana wetu na Mtume wetu Abil-Qasim Mustafa Muhammad, pamoja na Ahli wa nyumba yake waliowema watoharifu.
Maamkizi na amani ziuendee mkusanyiko ambao hivi sasa upo katika Msikiti Mtukufu wa Jamkaran.
Pamoja na kuyaenzi masiku ya baraka ya usiku wa Cheo(Qadr), natoa pole kutokana na shahada ya Hadhrat Amirul-Mu’minin Ali (a.s) na kuomba mwaka ujao uwe ni mwaka wa ushindi na hadhi kwa Waislamu wote, hasa Waislamu wa Iran na Mapinduzi ya Kiislamu kwa uwezo wa Mwenyezimungu.
Pasi na shaka Msikiti wa Jamkaran ni sehemu ya kipekee ambayo Imam Mahdi (a.f) anamtazamo wa maalumu kupahusu.
Unaporejea baadhi ya vyanzo utaona kwamba, Imam aliamuru ujenzi wa mahali hapa na kwa sababu hiyo, maulamaa wengi katika karne mbalimbali wamekuwa wakitilia umuhimu mkubwa juu ya sehemu hii takatifu.
Nafsi yangu inashuhudia kuwa kila nilipofanikiwa kutembelea msikiti huu, niliweza kupata mwelekeo mpya na hali nzuri, huku sala na maombi yangu yakipata kujibiwa, watu wengi wa hadhi ya juu pia wamezungumzia uzoefu wao katika msikiti huu wenye nuru, na nilisikia kutoka kwa baadhi ya maulamaa kuwa katika msikiti huu haja na matatizo mengi yamepatiwa ufumbuzi.
Tangia nilipokuja Qum mwaka 1322, sehemu hii ilikuwa ni maalum kwangu kwa ajili ya kutawasali na Imam wa zama (a.s).
Bila shaka, sehemu ambayo hujumuisha nyoyo za waumini na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) ina sifa za kipekee na inapaswa kupewa umuhimu, katika miaka ya hivi karibuni msikiti huu umepewa haki na kipaumbele zaidi kuliko awali, hasa ningependa kumshukuru kwa juhudi za kipekee Hujjatul-Islam na Muslimin Bwana Ajagh Nejad, ambaye kwa ufanisi na uchaji Mungu wake alianzisha kazi za kiutamaduni zilizo na faida katika kipindi hiki, kazi ambazo zilikuwa muhimu sana.
Na nilazima kwamba msikiti huu uwe ni kituo kikubwa cha kitamaduni na kwa ushirikiano na Hauza, pia ibadilishwe kuwa ni taasisi ya kielimu huku shughuli za kimataifa zikiendelezwa na kuzidishwa.
Mwisho, kwa heshima na taadhima katika viwanja vyenye nuru ya Imam wa zama (a.s), nawaombea Taufiq wapenzi wangu wote hapa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na vile vile ninawaomba mniombee Dua za kheri.
Qum Al-Muqaddasa
Hussein Nouri Hamedani
Maoni yako