Jumamosi 17 Oktoba 2026 - 11:50
Iran ikikabiliwa na tishio dhidi ya uwepo wake, hatutabaki watazamaji/ Tutaendelea kubaki katika safu ya Muqawama hadi uvamizi utakapokoma

Hawza/ Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada Iraq, huku akitoa onyo dhidi ya hatua zozote za kichokozi zinazolenga kuathiri ukamilifu wa ardhi na uwepo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesisitiza kuwa Muqawama wa Iraq hautabaki watazamaji endapo kutatokea tishio la kweli dhidi ya Iran, bali utaingia moja kwa moja katika safu ya ulinzi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika mahojiano na vyombo vya habari kuhusu mkakati wa vikosi vya Muqawama katika mabadiliko yanayoendelea katika eneo hili, Haj Abu Alaa al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, amesema: “Ikiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakabiliwa na tishio la msingi na la kweli dhidi ya uwepo wake, hatutabaki kamwe kuwa watazamaji wa matukio yanayoendelea. Badala yake, bila shaka tutakuwepo katika mstari wa mbele na katika safu ya kuilinda.”

Al-Wala’i ameueleza mkakati wa Muqawama kuwa ni kulinda kwa upana haki za Umma wa Kiislamu na watu wanaodhulumiwa duniani. Ameongeza kuwa: “Msingi na chimbuko la hatua zetu ni kushiriki kikamilifu katika kulinda umoja na ukamilifu wa Umma wa Kiislamu, kuunga mkono haki na kuwasaidia wanaodhulumiwa dhidi ya uchokozi.”

Akisisitiza kuwa njia ya Muqawama haiwezi kuyumbishwa, Al-Wala’i amesema: “Msimamo na mwenendo wetu wa kudumu ni kusimama imara na kuendeleza Muqawama. Maadamu damu bado inatiririka katika mishipa yetu, na maadamu eneo hili linaendelea kuwa chini ya kivuli cha uvamizi na anga yake kuwa uwanja wa vitendo vya uasi na jeuri vya wavamizi, hatutapotoka kamwe katika njia ya Muqawama.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha