Jumamosi 17 Oktoba 2026 - 12:50
Kusini mwa Lebanon chini ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni; wakulima wazuiwa kuvuna zaituni na vikwazo vya kilimo vyaendelea

Hawza/ Jeshi la kigaidi la utawala wa Kizayuni linaendelea kufanya mashambulizi ya angani na ya mizinga kusini mwa Lebanon. Sambamba na mashambulizi hayo, jeshi hilo limeing’oa miti ya zaituni katika eneo la Kafr Shuba na kuwazuia wakulima kuvuna mazao yao. Wakati huohuo, raia watatu pia waliuawa kishahidi katika maeneo hayo siku za Jumapili na Jumatatu zilizopita.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya kusini mwa Lebanon yanaendelea wakati ambapo msimu wa mavuno ya zaituni umefika, huku wakulima wakikabiliwa na vikwazo vikubwa. Mashambulizi ya angani, mashambulizi ya mizinga na operesheni za kubomoa mali yameathiri maeneo kadhaa.

Siku ya Ijumaa, tingatinga moja la utawala wa Kizayuni unaokalia kwa mabavu maeneo ya Lebanon, likiambatana na magari kadhaa ya kijeshi, liling’oa miti ya zaituni katika kijiji cha Kafr Shuba, kilichopo katika wilaya ya Hasbaya. Siku ya Alhamisi, vikosi vya kigaidi vya utawala huo vilikuwa vimewafukuza wakazi wa eneo hilo, licha ya kuwaahidi kwamba wangeweza kurejea katika eneo hilo wiki iliyofuata kwa ajili ya kuvuna zaituni.

Katika eneo hilo hilo, maeneo yanayozunguka shamba la Shunuh, lililopo pembezoni mwa maeneo ya Halta na Kafr Shuba, nayo yalishambuliwa kwa mizinga.

Katika kipindi hiki ambacho msimu wa mavuno ya zaituni umefikia kilele chake, vikosi vyenye silaha vya utawala huo vinaendelea kuwazuia wakazi kufanya shughuli za kilimo katika mashamba yao yaliyopo ndani ya eneo linalokaliwa kwa mabavu, ambalo lina ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 600.

Kuhusiana na hali hiyo, siku za Jumapili na Jumatatu zilizopita, raia watatu waliuawa kishahidi ndani au pembezoni mwa eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu, walipokuwa katika bustani zao za zaituni. Walifariki kutokana na mabomu na vilipuzi ambavyo havikuwa vimelipuka au kutokana na mashambulizi ya mizinga.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha