Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, ukimya wa kimataifa kuhusu mauaji yanayofanywa na adui wa Saudia nchini Yemen umegeuka kuwa kizuizi kinachochangia kuimarisha hali ya kutoadhibiwa kwa wahusika wa uhalifu huo.
Tangu kumalizika kipindi cha kupunguza mvutano, tarehe 23 Tir iliyopita, hadi tarehe 19 Mehr ya mwaka huu, idadi ya raia waliouawa na kujeruhiwa imeongezeka na kufikia watu 259, wakiwemo mashahidi 91 na majeruhi 168. Wanawake na watoto wanaunda takribani asilimia 60 ya wahanga hao.
Sambamba na mauaji yanayotokea kila siku, wavamizi wanaendelea kuharibu miundombinu muhimu, jumla ya shule na vituo vya elimu 1,400, pamoja na hospitali na vituo vya huduma za afya 436, vimeharibiwa, jambo linalokiuka waziwazi Mikataba ya Geneva na sheria za kimataifa za kibinadamu.
Katika kukabiliana na hali hii ya machafuko, Yemen inasisitiza haki yake halali ya kujilinda kwa mujibu wa Ibara ya 51 ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, pamoja na kanuni ya “kuzingirwa na kuongezeka mvutano kwa kuongezeka mvutano” hadi pale uchokozi utakaposimamishwa, mzingiro utakapoondolewa na uwajibikaji wa kimataifa utakapotekelezwa.
Idadi ya Raia Waliouawa na Kujeruhiwa Yafikia 259
Tangu kumalizika kipindi cha kupunguza mvutano nchini Yemen, tarehe 23 Tir H.S, ya mwaka huu na kuingia katika hatua ya kutekeleza kanuni ya “kuzingirwa na kuongezeka mvutano kwa kuongezeka mvutano”, idadi ya watu waliouawa na kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya Saudia imefikia 259 hadi tarehe 19 Mehr ya mwaka huu.
Takwimu hizo zimetangazwa na Dkt. Anis al-Asbahi, msemaji rasmi wa Wizara ya Afya ya Umma, Idadi ya Watu na Mazingira. Al-Asbahi amefafanua kuwa idadi hiyo inajumuisha mashahidi 91 na majeruhi 168, huku wanawake na watoto wakiunda takribani asilimia 60 ya wahanga wote.
Katika mahojiano yake na tovuti ya Ansarullah, Al-Asbahi amesisitiza kwamba; kulenga utaratibu masoko, sherehe za harusi na mikusanyiko ya raia nchini Yemen katika kipindi cha miaka 12 ya uchokozi wa Saudia kunafichua sera ya kuwatisha raia kwa ujumla. Lengo la sera hiyo ni kusababisha vifo na majeraha mengi iwezekanavyo miongoni mwa raia, wakiwemo wanawake na watoto.
Ameeleza kuwa; vitendo hivyo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu, na hivyo vinahitaji uchunguzi wa kimataifa pamoja na wahusika kuwajibishwa kisheria.
Uharibifu wa Shule na Vituo vya Elimu
Katika juhudi za kuweka kumbukumbu za madhara yaliyosababishwa kwenye mali na miundombinu ya huduma za kiraia, Al-Asbahi amebainisha kuwa; katika kipindi cha miaka kumi ya uchokozi, shule na vituo vya elimu vimeharibiwa au kuathiriwa kwa namna mbalimbali, na kufanya jumla yake kufikia shule na vituo vya elimu 1,400.
Hali hiyo imewanyima maelfu ya watoto haki ya kupata elimu na kuchangia kuongezeka viwango vya kuacha shule pamoja na watu kulazimika kuyakimbia makazi yao ndani ya nchi. Aidha, baadhi ya shule zilishambuliwa wakati wanafunzi walipokuwapo ndani yake, hali kusababisha vifo vya wanafunzi na walimu.
Al-Asbahi ameongeza kuwa; mashambulizi ya mabomu na uharibifu vimezikumba hospitali na vituo vya afya 436. Hali hiyo imeambatana na kuzuiwa dawa na vifaa vya matibabu kuingia nchini kutokana na mzingiro, jambo lililosababisha mfumo wa afya kukaribia kuporomoka kabisa na kuongeza vifo vinavyotokana na ukosefu wa huduma za matibabu.
Kwa mujibu wa Al-Asbahi, ukiukaji huu ni hatari maradufu kwa sababu unadhoofisha haki za raia kupata elimu na huduma za afya. Haki hizo mbili zinalindwa na kanuni za sheria za kimataifa za kibinadamu pamoja na Mikataba ya Geneva, ambayo pia inalenga kulinda hospitali na miundombinu ya kiraia.
Ameeleza kuwa kulenga shule, hospitali, nyumba, maeneo ya makazi, masoko na mikusanyiko ya raia hakuishii tu katika kusababisha hasara za maisha na mali. Badala yake, kwa kuinyima jamii fursa ya kupata elimu na huduma za afya, na kufanya juhudi za ujenzi upya kuwa ngumu zaidi, mashambulizi hayo yanailemaza jamii nzima. Kwa sababu hiyo, matukio haya yanapaswa kuchunguzwa na waliohusika wawajibishwe kisheria.
Wahanga wa Uchokozi na Mzingiro Wafikia Zaidi ya 54,000
Kwa upande mwingine, Ahmad Abu Hamra, mkuu wa Kituo cha Haki na Maendeleo cha Ayn al-Insaniyyah, amesisitiza kuwa; jumla ya raia walioathiriwa moja kwa moja na uchokozi na mzingiro wamefikia watu 54,219, wakiwemo mashahidi 19,446 na majeruhi 34,773.
Katika mahojiano yake na tovuti ya Ansarullah, amefafanua kuwa; mashambulizi hayo yameathiri vituo vya afya, taasisi za elimu, viwanja vya ndege, bandari, makazi, pamoja na sekta za uchumi na kilimo.
Amesema kuwa; jumuiya ya kimataifa, serikali ya Marekani na nchi zinazounda muungano wa kijeshi zinawajibika kwa matokeo ya mzingiro huo. Abu Hamra amesisitiza tena haki halali ya Yemen ya kujilinda na kulinda mamlaka yake ya kujitawala, huku akitoa wito wa kuondolewa mzingiro, kusimamishwa uchokozi na kufikishwa mahakamani wahusika wa uhalifu huu. Amesema hatua hizo ni utangulizi muhimu wa kufikia amani ya haki na inayojumuisha pande zote.
Maoni yako