Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Idara ya Mahusiano na Vyombo vya Habari ya Hizbullah imesema katika taarifa yake kuhusu tukio la eneo la Ghaleri Samaan kwamba kundi hilo halina uhusiano wowote na ghala lililotajwa wala vilivyomo ndani yake.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mahusiano na Vyombo vya Habari ya Hizbullah
Ili kufafanua mazingira ya tukio lililotokea katika eneo la Ghaleri Samaan, pamoja na habari na taarifa za kupotosha zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu suala hilo, Idara ya Mahusiano na Vyombo vya Habari ya Hizbullah inapenda kueleza kwamba; tukio hilo lilitokana na hatua ya doria moja ya vikosi vya usalama kuvamia eneo ambalo lina umuhimu na unyeti wa kiusalama, bila kuzingatia utaratibu uliokubaliwa kati ya Hizbullah na mamlaka za usalama.
Utaratibu huo unazingatia hali nyeti ya kiusalama katika kitongoji cha kusini mwa Beirut, kutokana na kuendelea vitisho na hatari za kiusalama kutoka kwa utawala wa “Israel”, pamoja na changamoto na vikwazo vinavyotokana na hali hiyo. Pande zote mbili zinatambua umuhimu wa kuielewa hali hiyo na kuwajibika ipasavyo kuhusiana nayo.
Baada ya mawasiliano muhimu kufanyika na mamlaka husika pamoja na taasisi za kisheria, na baada ya kubainika undani wa tukio hilo, doria hiyo ilikamilisha jukumu lake kwa utaratibu wa kawaida na kwa utulivu kamili, kwa ajili ya kutekeleza amri iliyotolewa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali, kufuatia rufaa iliyowasilishwa na Waziri wa Afya wa Umma, Rakan Nassereddine. Jeshi la Lebanon lilipowasili eneo hilo, hali ilikuwa tayari imerejea katika utaratibu wake wa kawaida.
Idara ya Mahusiano na Vyombo vya Habari ya Hizbullah inasisitiza kwamba kundi hilo halina uhusiano wowote, wa karibu wala wa mbali, na suala la ghala lililotajwa au vilivyomo ndani yake.
Kama ambavyo Hizbullah inajali afya na usalama wa raia na kuunga mkono hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Afya, pia inasisitiza umuhimu wa vikosi vya usalama kutekeleza majukumu na wajibu wao wa kawaida.
Idara ya Mahusiano na Vyombo vya Habari ya Hizbullah
Ijumaa, 24 Mehr 1405 Hijria Shamsia (16 Oktoba 2026 Miladia / 4 Jumada al-Awwal 1448 Hijria Qamaria).
Maoni yako