Alhamisi 8 Oktoba 2026 - 09:00
Imam Khamenei Shahidi: “Tufan Al-Aqsa Ilifuta Mipango Mikubwa ya Adui Katika Eneo”

Hawza/ Imam Khamenei Shahidi, huku akizungumzia operesheni ya  Tufan Al-Aqsa, ameitaja operesheni hiyo kuwa ni hatua ya kuamua na iliyokuwa ikihitajika katika eneo, ambayo kwa kuvuruga njama kubwa ya kimataifa iliyokuwa imepangwa Asia Magharibi, iliupiga utawala wa Kizayuni pigo lisiloweza kurekebishwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya tarehe 7 Oktoba, tunawaletea baadhi ya kauli za Sayyid Shahidi wa Mashahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khamenei Shahidi, kuhusu suala hili.

Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi: Tufan Al-Aqsa Illitokea Kwa Wakati Wake Haswa na Kuyeyusha Mipango ya Adui “Sababu inayowafanya muuone utawala wa Kizayuni ukiwashambulia kwa ukali na ukatili mkubwa watu wasio na ulinzi wa Ghaza, ni mwitikio wa jazba wa utawala huo kutokana na kubatilishwa kwa mpango huo. Na sababu inayowafanya muione Serikali ya Marekani, mbele ya macho ya watu wote duniani, ikiisaidia katika uhalifu huu, ni kutokana na mwitikio wao wa jazba kwa kubatilishwa kwa mpango ambao walikuwa wameuchora kwa juhudi kubwa. ‘Tufani ya Al-Aqsa ilifanya muujiza wa aina hiyo.’”

“Tufani ya Al-Aqsa Al-Aqsa ilitokea kwa wakati wake hasa na katika dakika yake mwafaka. Kwa hakika, siwezi kudai kwamba waliounda na kupanga Tufani ya Al-Aqsa walijua au hawakujua ni kazi kubwa kiasi gani waliyokuwa wakiifanya — mimi sijui — lakini ukweli ni kwamba hatua waliyoichukua ilikuwa ni hatua ambayo hakuna jambo jingine lingeweza kuchukua nafasi yake; waliondoa na kubatilisha kupitia operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa njama kubwa ya kimataifa iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya eneo la Asia Magharibi.”

“Operesheni hii ya Tufani ya Al-Aqsa ilikuwa hasa ndiyo iliyohitajika katika eneo hili; eneo letu lilikuwa likihitaji operesheni hii.”

“Operesheni hii lilikuwa pigo la kuamua dhidi ya utawala wa Kizayuni; pigo ambalo hakuna tiba wala suluhisho kwa ajili yake, na utawala wa Kizayuni, kutokana na pigo hili, umekumbwa na matatizo na majanga ambayo hautaweza kuokoka kuepukana nayo.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha