Ijumaa 2 Oktoba 2026 - 14:00
Watawala wa nchi za Kiarabu wameichagua Marekani kuwa Mola wao

Hawza/ Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain ametoa tamko kuhusu wajibu wa mataifa mbele ya tawala ambazo zimeichagua Marekani kuwa Mola wao, na kuwataka wananchi kusimama dhidi ya tawala hizo na kukabiliana nazo.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sheikh I'sa Qassim, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain, katika tamko lililochapishwa na ukurasa wa “Mawqi‘ al-Muqawim”, amezitaka jamii za nchi za Kiarabu, Kiislamu na mataifa mengine yaliyo chini ya utawala wa Marekani kukabiliana na tawala rasmi zinazotawala, ambazo zimeichagua Marekani badala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa Mola na muabudiwa wao.

Ayatullah Qassim amesema: “Enyi wananchi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, na enyi wananchi wengine mnaokabiliwa na utawala wa Marekani! Zungumzeni na tawala rasmi zinazowatawala, ambazo zimeichagua Marekani badala ya Mwenyezi Mungu kuwa Mola na muabudiwa wao, na ambazo kwa uaminifu na utiifu wa moja kwa moja, au kwa mali, mikono na nafsi, na kwa kuwasukuma watoto wao katika njia hii ya uaminifu na kutoa mali na nafsi zao kwa ajili ya kumuunga mkono huyo muabudiwa wa uongo, ambaye katika vita vyake vyote vya kidhalimu na upanuzi wake wa dhuluma katika maeneo yote ya dunia hutumia nguvu batili kwa ajili ya kuzikandamiza serikali na mataifa.”

Ameyataka mataifa yasimame dhidi ya tawala hizo na kuyaambia: “Mola wenu asiye na ujuzi na mwenye kiburi, ambaye mmemchagua badala ya Mwenyezi Mungu wa kweli kuwa Mola wenu, ni dhalimu asiye na uadilifu; ni katili asiye na huruma; ni mwenye tamaa asiye na mipaka; ni dikteta asiye na mwisho; ana kiu ya damu; anadharau heshima na anakufuru dhidi ya thamani na utu wa mwanadamu. Katika marafiki zake, yeye hawaoni isipokuwa watumwa wanaomtii yeye na wafuasi wake watiifu; watumwa ambao ameweza kuwatumia kwa ajili ya kupandisha malengo yake duni, kutosheleza hulka zake zilizo na maradhi na kutekeleza maovu yake ya moja kwa moja.”

Ayatullah Qassim ameongeza kusema: “Waambieni kwamba ikiwa mtaendelea na njia hii kwa kuacha mahusiano yote ya kidini, thamani, hisia za heshima na sifa za kibinadamu, na mkafanya hivyo kwa ajili tu ya kulinda kiti chenu kinachotikisika na hisia yenu ya udanganyifu ya kuwa na utawala wa uongo juu ya taifa hili lililodhoofishwa au lile, basi yote haya yanapingana na maumbile safi, akili yenye afya, hisia zenye thamani na shauku ya kufikia ukamilifu ambayo Mwenyezi Mungu amewajaalia waja Wake.”

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain pia amekosoa tawala zinazotawala ambazo zinajiweka zenyewe pamoja na uwezo na rasilimali zao zote chini ya wale ambao wanajua kwa yakini kwamba matakwa yao pekee katika maisha haya ni kumdhalilisha kila mtu na kuvunja matakwa na misimamo yao. Aidha, ametoa tahadhari kwamba: “La sivyo, matokeo yatakuwa ni vita tu, kuvunjwa na kusambaratishwa, moto mkubwa na uharibifu, ambao hautofautishi kati ya mwenye amani na mpiganaji, mdogo na mkubwa, wala aliye karibu na aliye mbali; na ni machafuko yanayoharibu maisha.”

Sheikh Isa Qassim, akionya kuhusu madhara ya mataifa kunyamaza au kuchelewa kusema neno la haki, amesema: “Iwapo mataifa hayatatoa kauli yao [dhidi ya dhuluma hii], au yakachelewa kuitaja kwa wakati wake, basi uhalifu wao dhidi yao wenyewe utakuwa mkubwa usioweza kupimika. Enyi watu, nyote muwe macho na mpate uelewa, kabla ya muda haujapita.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha