Jumatano 25 Novemba 2026 - 12:50
Ayatollah Arafi Amewasilisha Rambirambi Zake kwa Ayatollah Sheikh Isa Qassim

Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mke wa Ayatollah Sheikh Isa Qassim.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, matini ya ujumbe wa rambirambi wa Ayatollah Alireza Arafi aliomwelekezea Ayatollah Sheikh Isa Qassim ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

«كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ»

“Kila nafsi itaonja mauti.”

Mtukufu Ayatollah Haj Sheikh Isa Ahmad Qassim,

Ninawasilisha kwako salamu zangu za dhati za rambirambi kufuatia kufariki mke wako mtukufu.

Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amteremshie rehema Zake marehemu huyo mwanamke mtukufu, na akujaalie wewe pamoja na ndugu na jamaa wengine wote waliobaki subira njema na ujira mkubwa.

Alireza Arafi
Mkurugenzi wa Hawza za kielimu nchini Iran

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha