Jumamosi 5 Septemba 2026 - 09:26
Safari ya Kielimu ya Ayatullah Karbasi Kuelekea Amerika Kusini kwa Lengo la Kufanya Mazungumzo ya Kidini na Kuimarisha Mawasiliano na Wafuasi wa Ahlulbayt (as)

Hawza/ Ayatullah Sheikh Muhammad Swa'diq Muhammad Karbasi, mwandishi wa “Ensaiklopidia ya Imam Hussein” na Mkuu wa “Kituo cha Tafiti za Imam Hussein” mjini London, amewasili katika nchi za Amerika Kusini katika safari maalumu yenye lengo la kutembelea vituo na Husainiya.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sheikh Muhammad Swa'diq Muhammad Karbasi, mwandishi wa “Ensaiklopidia ya Imam Hussein” na Mkuu wa “Kituo cha Tafiti za Imam Hussein” mjini London, amewasili katika nchi za Amerika Kusini katika safari maalumu iliyolenga kutembelea vituo na Husainiya, kukutana na Waislamu na wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt (as), pamoja na kuchunguza hali ya Uislamu katika eneo hilo.

Ayatullah Karbasi alianza ziara yake nchini Paraguay, ambako maandalizi yanaendelea kwa ajili ya ratiba yenye shughuli nyingi na mikutano maalumu, kufuatia mialiko na mawasiliano mengi aliyoyapokea kutoka kwa vituo vya utafiti na Kiislamu katika nchi mbalimbali za Amerika Kusini.

Ayatullah Karbasi alisisitiza: Safari hii inafanyika katika mfumo wa kujenga madaraja ya mawasiliano ya kielimu na kiroho na jamii za Kiislamu zilizo katika nchi za ugenini, pamoja na kupata ufahamu wa moja kwa moja kuhusu mahitaji ya vituo vya kidini na kiutamaduni.

Aliendelea kusema: Safari hii pia inalenga kuimarisha uwepo wa wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbayt (as) katika bara la Amerika Kusini, na kuchunguza njia za kuamsha na kuendeleza mazungumzo ya kidini yenye msimamo na uimara ambayo yanaendelezwa na Ensaiklopidia ya Imam Hussein.

Inafaa kutajwa kwamba Ayatullah Karbasi hapo awali pia alifanya safari pana ya kielimu katika bara la Ulaya, iliyoanzia katika mji mkuu wa Uingereza, London, na kumalizikia huko huko. Safari hiyo ilihusisha kutembelea nchi 34 za Ulaya kwa muda wa siku 45, katika majira ya machipuko ya mwaka 2019 Miladia (1398 Hijria Shamsia).

Ayatullah Karbasi aliandika kwa kina safari hiyo ya Ulaya kwa mtindo wa kina na uliopangiliwa kwa kuzingatia ratiba ya kila siku. Aliambatanisha maelezo ya moja kwa moja kuhusu hali ya barabara, mazungumzo aliyofanya na shakhsia mashuhuri za Kiislamu, pamoja na ziara za moja kwa moja katika misikiti, vituo na Husainiya.

Kazi hiyo ilikuwa na sifa ya kipekee ya kifasihi, kiasi kwamba mwandishi alikuwa akihitimisha kumbukumbu ya ziara yake katika kila nchi kwa shairi alilolitunga mwenyewe, ambalo lilikuwa likielezea nchi hiyo na kugusia kwa kina mambo mbalimbali kuihusu.

Maelezo ya safari hiyo pana ya kielimu yamechapishwa kwa mfululizo katika juzuu kadhaa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha