Alhamisi 3 Septemba 2026 - 14:09
Shule ya Msingi ya Kiislamu Yafunguliwa Tena Edmonton, Canada

Hawzah/ Kwa kuanza mwaka mpya wa masomo nchini Canada, shule binafsi ya Edmonton imefungua milango yake kwa wanafunzi kutoka katika makundi yote. Shule hiyo ya msingi inafuata masomo ya kawaida yaliyoainishwa na mfumo wa elimu wa Canada, huku masomo ya Kiislamu na Qur’ani yakifundishwa kama nyongeza.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, tawi jipya la Shule ya Msingi ya Kiislamu ya Edmonton limefungua milango yake kwa wakati mwafaka, likiukaribisha mkondo mpya wa wanafunzi wenye asili na madhehebu mbalimbali.

Kufunguliwa kwa shule hii binafsi iliyopo magharibi mwa Edmonton ni hatua muhimu katika uwepo wa Edmonton Islamic Academy ndani ya jamii ya Canada, ambayo imejengeka kwa miongo kadhaa. Mtaala wa shule hii unafuata miongozo ya kielimu ya mkoa, huku wakati huohuo ukijumuisha masomo ya Kiislamu, Qur’ani na lugha ya Kiarabu.

Imepita takribani miaka 90 tangu taasisi hii ianze shughuli zake. Mwanzoni, ilianza kazi zake katika msikiti uliokuwa ukitumika kwa shughuli mbalimbali za kitamaduni nchini Canada, unaojulikana kwa jina la Msikiti wa Al-Rashid.

Awali, sherehe kubwa ya ufunguzi ilifanyika kwa kuhudhuriwa na wanafunzi, familia, wahitimu na walimu. Aidha, waliohudhuria walitembelea eneo la uchimbaji na ujenzi mpya unaofanyika kwa ajili ya upanuzi wa shule hiyo.

Benjamin J., mwalimu wa darasa la tatu ambaye amekuwa akifundisha katika taasisi hii tangu ilipoanza shughuli zake, alisema siku ya Jumamosi: «“Kituo hiki ni kizuri sana. Ni kipya kabisa na kinang’aa, lakini nadhani jambo muhimu zaidi ni kwamba kiwe sehemu salama kwa wanafunzi wetu kujifunza.”»

Chanzo: ctvnews.ca

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha