Shirika la Habari la Hawza – Muni Ovadia, mwigizaji, mwimbaji, mwandishi na mwanafikra Myahudi mwenye asili ya Italia, alizungumza kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati katika kipindi cha televisheni cha uchambuzi “In Onda”, kilichorushwa tarehe 24 Agosti 2026 (2 Shahrivar 1405), ambapo alichukua msimamo wa wazi na wa ujasiri wa kuikosoa vikali itikadi ya Uzayuni pamoja na sera za utawala wa Tel Aviv.
Muni Ovadia: “Unaweza kutarajia kila jambo kutoka kwa Netanyahu na Wazayuni. Tunakabiliana na mtazamo wa kihalifu...”
Mtangazaji (Luka Teleze): “Wewe, kama Myahudi, unatumia neno ‘Mzayuni’ kama sifa yenye maana hasi?”
Muni Ovadia: “Ndiyo. Na sitaki tena kamwe kusikia ikitajwa ‘Dola ya Kiyahudi’ au ‘Dola ya Israel’. Kwa mtazamo wangu, hii ni dola ya Kizayuni iliyojengwa juu ya itikadi ya kihalifu, ya kikoloni, ya ubaguzi wa mfumo wa Apartheid, ya kibaguzi wa rangi na hatimaye ya mauaji ya kimbari.
“Kwa mtazamo wangu, hii ndiyo tafsiri inayoweza kukubalika katika zama hizi. Ninasema haya nikiwa Myahudi.
“Mimi, kama Myahudi, ninakataa aina yoyote ya kuhusisha Uzayuni na Uyahudi. Mimi si muumini.”
Maoni yako