Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Kamanda wa Jeshi la Lebanon, Jenerali Rodolph Haykal, wakati wa ziara yake katika kikosi cha Kumi na Moja ya Jeshi cha Miguu katika eneo la Naqqash, pamoja na Vikosi vya Uingiliaji vya Tatu vilivyoko Manara na Vikosi vya Nne katika Kambi ya Kijeshi ya Henry Chehab, alisisitiza kuwa; kuchochea fitina za ndani ni mojawapo ya malengo ya utawala vamizi wa Israel na kwamba ni lazima njama hizo zikabiliwe.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuendelea na mafunzo pamoja na kuimarisha uwezo wa vikosi vya jeshi, katika mazingira ya changamoto ambazo Lebanon inakabiliana nazo.
Baada ya kupata taarifa kuhusu hali ya utayari wa kiutendaji wa vikosi hivyo, Haykal alikutana na maafisa pamoja na wanajeshi. Akiwapongeza kwa maadhimisho ya Siku ya Jeshi, alisema: Taasisi ya kijeshi imesimama imara kutokana na juhudi zenu kubwa, na inaendelea kutekeleza majukumu yake katika moja ya vipindi vigumu zaidi katika historia ya taifa.
Pia alisema: Mapenzi ya wananchi wa Lebanon kwa jeshi lao na imani waliyonayo kwalo ni matokeo ya kujitolea kwa wanajeshi katika maeneo mbalimbali wanayohudumu.
Maoni yako