Jumamosi 1 Agosti 2026 - 12:43
Ustahimilivu ni somo kubwa la Arubaini katika zama zetu za leo

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qom amesema: Arubaini ina mafunzo makubwa, na miongoni mwa mafunzo hayo ni ustahimilivu. Imam Hussein (as) kupitia harakati yake alibainisha kwamba; kipimo cha ushindi hakiko katika kuendelea kuwepo kwa sura ya nje, bali katika kutimia malengo ya Mwenyezi Mungu na kuleta mpasuko katika mfumo wa utawala wa kitwaghuti. Ushindi ambao hatimaye ulisababisha kuanguka kwa Bani Umayya, ukaamsha mwamko wa Kiislamu na kuwa mfano kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa hirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saiidi, katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 9 Mordad 1405 (July 31 2026) zilizofanyika Muswalla Quds mjini Qom, alisema kuwa: Sherehe za Arubaini huwafundisha wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) somo la uchamungu. Kusimama katika njia ya Mwenyezi Mungu, kuwa thabiti na kuvumilia katika njia Yake, kutorudi nyuma katika njia ya Imam Hussein (as), na kutowaamini maadui na wanafiki ni miongoni mwa matunda ya uchamungu wa kivitendo unaofundishwa ndani ya Arubaini.

Khatibu wa Swala ya Ijumaa wa Qom aliendelea kusema: Arubaini ina mafunzo makubwa, na miongoni mwa hayo ni ustahimilivu. Imam Hussein (as) kupitia harakati yake alibainisha kwamba kipimo cha ushindi hakiko katika kuendelea kuwepo kwa sura ya nje, bali katika kutimia malengo ya Mwenyezi Mungu na kuleta mpasuko katika mfumo wa kitw'aghuti. Ushindi huo ulifuatiwa na kuanguka kwa Bani Umayya, ukasababisha mwamko wa Kiislamu na kuwa mfano kwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Alisema: Imam Hussein (as) ametufundisha kwamba kusimama imara mbele ya adui, kwa gharama yoyote ile, bila shaka huleta ushindi wa mwisho, kwa sharti la kuwa na ustahimilivu. Kwa ajili ya kuhakikisha harakati ya Karbala inazaa matunda, Imam Hussein (as) alisema: «صَبْرًا بَنِي الْكِرَامِ», akionesha msingi wa ustahimilivu.

Imamu wa Ijumaa wa Qom alisema: Uwepo wa wananchi siku 150 kwa ustahimilivu na bila kuchoka, pamoja na ushiriki wa mamilioni ya watu katika matembezi ya Arubaini, ni miongoni mwa vielelezo vya mafunzo ya mwezi wa Muharram, Swafar na Arubaini.

Akirejelea Siku ya Redio na Televisheni alisema: Chombo cha habari cha taifa ni jeshi la habari la umma uliotumwa. Licha ya changamoto zilizopo, katika vita viwili vya karibuni vya kujihami, chombo hicho kimekuwa sauti ya umma uliotumwa, na kiling'ara katika kurusha moja kwa moja mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi. Aidha, katika jihadi endelevu ya habari hakijawahi kuiacha ngome yake hata kwa muda mfupi.

Msimamizi wa Haram ya Bibi Maasumah (as), kuhusu barua ya kiapo cha utii cha Hizbullah ya Lebanon kwa Imam wa Umma, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, alisema: Wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon walitoa kiapo cha utii kwa Imam wa Umma, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, kupitia barua. Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, akirejelea nafasi ya mbele ya Hizbullah ya Lebanon katika kupambana na utawala wa Kizayuni na wanaouunga mkono, alisisitiza kuendelea kwa sera ya kimkakati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuwatetea wapiganaji wa Lebanon, na akasema: "Leo, wakati mataifa duniani yamechoshwa na dhuluma na uonevu wa serikali ya Marekani pamoja na Wazayuni wahalifu wanaoharibu mimea na kizazi cha watu, hakuna njia nyingine iliyobaki isipokuwa jihadi na mapambano ya muqawama."

Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi mjini Qom, huku akitoa salamu za rambirambi kufuatia kuuawa kishahidi Brigedia Jenerali Msaidizi Rubani Majid Kazemi, alisema: Rubani huyu shujaa na jasiri, baada ya kutekeleza kwa mafanikio operesheni yake dhidi ya kambi ya Marekani katika eneo hilo, alishambuliwa na adui akiwa njiani kurejea juu ya Ghuba ya Uajemi na akapata daraja ya shahada.

Adui wa Kimagharibi, Kiebrania na Kiwahabi amekasirishwa na hatua za Hashd al-Shaabi

Alisema: Kufuatia mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Saudi dhidi ya kambi za Hashd al-Shaabi nchini Iraq, wimbi kubwa la kulaani shambulio hilo pamoja na wimbi la kuunga mkono jeshi hilo la wananchi limejitokeza katika eneo. Hashd al-Shaabi ni kikosi ambacho katika siku ngumu zaidi za uvamizi wa Daesh kilisimama kama ngome imara dhidi ya magaidi na kilikuwa na nafasi muhimu katika kuangamiza ugaidi wa kitakfiri na Kiwahabi. Pia walikuwa na nafasi kuu katika shughuli za mazishi ya mamilioni ya watu ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi nchini Iraq.

Imamu wa Ijumaa wa Qom aliendelea kusema: Hatua hizi ziliibua hasira za mhimili wa Kiebrania, Kimagharibi na Kiwahabi, kiasi kwamba usiku wa manane walifanya shambulio la kinyama dhidi ya kambi za Hashd al-Shaabi nchini Iraq na kuwaua kishahidi na kuwajeruhi idadi kubwa ya wanajeshi hao. Tunaitarajia serikali ya Iraq kuwalinda na kuwaunga mkono askari hawa waumini, waaminifu kwa uongozi, wenye heshima, waliodhulumiwa na wenye nguvu dhidi ya maadui wa kigeni na wanafiki mamluki wa ndani ya Iraq.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha