Jumamosi 13 Juni 2026 - 22:25
Mabadiliko ya Kivita na “Umoja wa Medani za Mapambano” Vamevuruga Hesabu za Kizayuni na Kimarekani nchini Lebanon na katika Ukanda Mzima

Hawza/ Mapambano katika eneo dhidi ya utawala wa Kizayuni yameingia katika hatua ngumu zaidi, dalili za kushindwa kwa utawala huo wa uvamizi zinazidi kujitokeza siku baada ya siku.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mapambano katika eneo dhidi ya utawala wa Kizayuni yameingia katika hatua ngumu zaidi, dalili za kushindwa kwa utawala huo wa uvamizi katika kutekeleza mipango ambayo ulikuwa umeibeba tangu mwanzo wa uchokozi wake dhidi ya Lebanon — iwe ni kusonga mbele kwa vikosi vya ardhini, sera ya uharibifu mkubwa au juhudi za kuleta maeneo matupu kando ya mipaka — zinazidi kuwa wazi siku baada ya siku.

Katika kukabiliana na ongezeko la mvutano kutoka kwa Israel, katika siku za hivi karibuni vikosi vya Muqawama katika eneo vimelazimisha kanuni mpya za mchezo wa kivita, ambapo mhimili wake mkuu ni kuzuia wavamizi kushughulikia kila uwanja wa mapambano kivyake au kuuweka kila mmoja chini ya shinikizo peke yake, hali hii imepelekea kufafanuliwa upya kwa sheria za mapambano kwa namna ambayo ongezeko lolote la mvutano kutoka kwa Israel linakabiliwa na majibu mapana zaidi; jambo ambalo limezua wimbi la wasiwasi unaoongezeka ndani ya taasisi za kijeshi na kisiasa za Israel.

Mabadiliko haya yamekuja sambamba na harakati za kisiasa na kidiplomasia za haraka kuhusu mustakabali wa vita na njia za kufikia usitishaji vita, wakati juhudi za kulazimisha makubaliano mapya zikiendelea, Muqawama bado unasisitiza kwamba; mpangilio wowote wa kisiasa hauwezi kutenganishwa na hali halisi ya medani za mapambano na mizani ya nguvu inayoundwa chini ya kivuli cha muqawama na operesheni za kijeshi zinazoendelea.

Katika muktadha huo, Brigedia Jenerali Ali Abi-Raad, mtaalamu wa masuala ya kijeshi na kimkakati, alisisitiza kwamba; operesheni ya kuvuka mipaka ya Lebanon na Palestina, yenyewe peke yake, inachukuliwa kuwa pigo kubwa kwa mfumo wa usalama na kijeshi wa Israel; kwa sababu imefichua udhaifu wa wavamizi katika kulinda eneo ambalo walidai kulidhibiti kikamilifu kupitia ngome, teknolojia za kisasa na uharibifu mkubwa katika ukanda wote wa mpaka.

Abi-Raad katika mahojiano yake na mtandao wa Al-Masirah alieleza kwamba; kabla ya makubaliano ya tarehe 27 Novemba 2024, wavamizi walikuwa wakijaribu kuunda eneo la juu la ulinzi ndani ya ardhi ya Lebanon kwa lengo la kulinda makazi ya walowezi wa kaskazini, vile vile waliendelea kushikilia vituo sita vya kijeshi ndani ya ardhi ya Lebanon na kujenga vituo vyao vya ngome huko. Hata hivyo, hatua zote hizo hazikuweza kuzuia hata mpiganaji mmoja kuingia ndani ya ardhi ya Palestina na kupambana na vikosi vya Israel bila mifumo ya ufuatiliaji na ujasusi ya Israel kugundua uwepo wake.

Alibainisha kwamba; hali ya mkanganyiko iliyoikumba Israel baada ya operesheni hiyo ilidhihirika katika mgongano wa simulizi za taasisi zake za habari na za kijeshi, pamoja na kushindwa kubaini iwapo operesheni hiyo ilifanywa na mtu mmoja au kundi. Jambo hili liliwalazimu kuviita vikosi maalumu vya “Shayetet 13” ili kufanya operesheni kubwa ya usafishaji katika eneo hilo.

Aliongeza kuwa; tukio hilo si la kwanza la aina yake, alikumbusha operesheni ya awali ambapo mmoja wa wapiganaji wa Muqawama aliweza kufika katika makazi ya walowezi ya Al-Qawzah — ambayo yalikuwa chini ya udhibiti kamili wa Israel — akamuua afisa mmoja wa Israel kisha akarudi salama, kwa maoni yake, jambo hili linaonesha kiwango kikubwa cha udhaifu wa usalama na kijeshi wa vikosi vya uvamizi.

Kuhusu ongezeko la hivi karibuni la mvutano kutoka kwa Israel, Abi-Raad anaamini kwamba; wavamizi wanajaribu kwa wakati mmoja kusonga mbele ardhini huku wakiongeza kiwango cha uharibifu na gharama za vita kusini mwa Lebanon. Kwa mtazamo wao, Marekani iko karibu kufikia makubaliano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hivyo wanajaribu kupata mafanikio makubwa kadiri wawezavyo kabla ya usitishaji vita wowote.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha