Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika hotuba za Swala ya Ijumaa alizotoa katika Husainiyya Kubwa ya Fatimiyya mjini Najaf Ashraf, katika kumbukumbu ya mwaka wa kumi na mbili tangia kuanguka kwa mji wa Mosul mwaka 2014 na kuachiliwa kwake ndani ya mwaka huo huo, alizungumzia nadharia ya undugu katika Uislamu na akauliza swali hili: Je, vipi Mashia wa Ahlul-Bayt (a.s) walipigana kwa ajili ya kuikomboa Mosul na Al-Anbar na wakatoa maelfu ya mashahidi katika njia hiyo?
Alijibu kwamba: Mashia wa Ahlul-Bayt (a.s) wanaamini katika undugu ndani ya Uislamu, kama ambavyo Mwenyezi Mungu anasema:
﴿إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ﴾
“Hakika Waumini ni ndugu.”
Pia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema:
«مَن لم یهتمَّ بأمور المسلمین فلیس منهم»
“Yeyote ambaye hajali mambo ya Waislamu basi si katika wao.”
Na Amirul-Muuminin Ali (a.s) amesema:
«الناسُ اثنان: أخٌ لک فی الدین، ونظیرٌ لک فی الخَلق»
“Watu wako katika makundi mawili: ama ni ndugu yako katika dini, au ni sawa na wewe katika maumbile.”
Aliongeza kuwa: Imam Sajjad (a.s) alikuwa akiwapa sadaka mafakiri, akaambiwa: “Hawa ni Makhawarij na wauaji wa babu yako!” Akajibu: “Ndiyo, na lau wasingekuwa hata Makhawarij, ningewapa mkate na chumvi.”
Kwa hiyo, wito wa kuwasiliana na kuonyeshana mapenzi upo, na hii ndiyo nadharia ya Mashia wa Ahlul-Bayt (a.s). Ndiyo maana Imam Khomeini (r.a) alilingania kwenye umoja wa Kiislamu, na Ayatullah Sistani alisema: “Msiseme ndugu zetu, bali semeni sisi wenyewe.”
Hapa pia msimamo ulikuwa ni msimamo chanya wa kuwaunga mkono Waislamu wa Ghaza. Ndiyo, kuna nadharia nyingine pia inayojengwa juu ya kutengana na uadui, lakini Ahlul-Bayt (a.s) hawaikubali nadharia hiyo.
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika muktadha huo huo, alikumbusha pia janga la walilopata vijana katika tukio la Speicher mnamo tarehe 12 Juni 2014, na kusema kwamba; sauti za kudai wahalifu wafikishwe mbele ya sheria bado zinaendelea kusikika kwa nguvu, ingawa baadhi ya maafisa wametangaza kwamba watu 72 miongoni mwa wauaji wamehukumiwa kunyongwa, bado makumi ya wahalifu wako nje ya mkono wa sheria.
Alilaani ukimya wa dunia na kusema: “Kuna matukio ambayo wanawake 19 walichomwa moto ndani ya mabanda ya chuma, lakini dunia haijawahi kuyazungumzia.”
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi, kuhusu masuala ya ndani ya Iraq, alisema: “Katika kipindi hiki cha kuelekea safari ya karibu ya Waziri Mkuu kwenda Marekani, tunatarajia Waziri Mkuu atake kuachiliwa kwa mapato ya mafuta ya Iraq; kwa sababu zaidi ya asilimia 95 ya mapato hayo yanawekwa katika Benki ya Shirikisho la Marekani, licha ya kwamba Iraq tayari imeondolewa chini ya Kifungu cha Saba. Kwa hiyo tunamtaka Mkuu wa Baraza la Mawaziri kudai kuondolewa kwa vikwazo juu ya mapato ya Iraq.”
Maoni yako