Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, taarifa kutoka Kuwait zinaonesha kuwa; mamlaka ya mahakama ya Kuwait imethibitisha hukumu iliyotolewa dhidi ya Zainab Dashti, mtangazaji wa televisheni rasmi ya Kuwait, Kwa mujibu wa hukumu hiyo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani kwa tuhuma za kuchochea fitna na kuathiri maslahi ya taifa.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya mashambulizi ya ukosoaji dhidi yake katika kipindi cha hivi karibuni; mashambulizi yaliyotokana na kuchukua baadhi ya misimamo na mitazamo ambayo alikuwa ameichapisha kupitia akaunti zake binafsi katika mitandao ya kijamii kuhusu vita, ambapo baadhi ya watu walitafsiri misimamo hiyo kama aina ya kuonesha mshikamano na Iran.
Maoni yako