Jumapili 7 Juni 2026 - 18:00
Jinai inayofanywa na adui dhidi ya jeshi la taifa imekuwa ni matokeo ya kawaida na ya kupuuzwa kwa mamlaka ya nchi

Hawza / Hizbullah katika taarifa yake imesema: Shambulio la kijinai na la woga ambalo adui Mzayuni amelifanya dhidi ya jeshi letu la taifa ni jinai ya kweli na ya makusudi.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah katika taarifa yake imesema: Shambulio la kijinai na la woga ambalo adui Mzayuni amelifanya dhidi ya gari la kijeshi la jeshi letu la taifa ni jinai ya kweli na ya makusudi.

Taarifa ya Hizbullah kuhusu uvamizi wa kijinai wa Kizayuni dhidi ya jeshi la Lebanon ni kama ifuatavyo:

Shambulio hilo la kijinai na la kinyonge ambalo adui Mzayuni amelifanya dhidi ya gari la kijeshi la jeshi letu la taifa, na ambalo limesababisha kuuawa kishahidi kwa maafisa wawili na askari mmoja, ni jinai halisi na ya makusudi ambayo imeongezwa katika orodha za jinai za adui dhidi ya wananchi wa Lebanon, hasa katika maeneo ya Kusini na Bonde la Magharibi la Biqaa.

Hatua hii ni matokeo ya kawaida ya kupuuzwa kwa mamlaka ya nchi, damu za wananchi, na upendeleo wa bure ambao serikali imekuwa ikitoa; ikiwemo tukio la hivi karibuni la kujisalimisha kikamilifu kwa serikali mbele ya masharti ya adui huko Washington, jambo ambalo limempa adui ujasiri wa kuendelea kumwaga damu dhidi ya wananchi na jeshi letu.

Hizbullah huku ikitoa pole za dhati na kuonesha mshikamano wake na familia za mashahidi wa jeshi pamoja na taasisi ya kijeshi — kuanzia makamanda, maafisa hadi askari — imelaani uvamizi huu wa kihalifu na kusisitiza kuwa itasimama bega kwa bega pamoja na jeshi la taifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha