Jumatano 3 Juni 2026 - 15:10
Mihimili 18 ya Dhahabu katika Khutba ya Ghadir

Hawza/ Marehemu Ibn Jabr aliyefariki katika karne ya saba Hijria katika kitabu chake chenye thamani kubwa Nahj al-Iman, ameeleza khutba yenye urefu wa wastani kuhusu kuelezea hadhi, nafasi na daraja la mtukufu huyo, na ametaja neno “Ma'ashir an-Nas” (Enyi watu) takribani mara 70; jambo ambalo ni ushahidi bora kabisa wa kimataifa wa maneno ya Mtume huyo mtukufu wa Mwenyezi Mungu, haya yalikuwa maneno ambayo yalielekezwa kwa watu wote kwa ujumla na hayakuhusishwa na kundi maalumu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Muhammad Jaafar Muruji Tabasi katika makala yenye anwani “Lulu za Maarifa ndani ya Khutba ya Ghadir” ameandika:

Siku ya kumi na nane ya mwezi wa Dhul-Hijjah ni siku ya kutawazwa Kiongozi wa Wachamungu Amirul-Muuminin Ali (as) kupitia Mtume Mtukufu wa Uislamu.

Katika siku hii yenye maamuzi makubwa ambayo inahusiana na mustakabali wa Umma wa Kiislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alitoa maneno muhimu sana kuhusu ubora wa Kiongozi wa Wachamungu katika hali ya joto kali na katika jangwa lisilo na maji wala mimea.

Joto lilikuwa kali kiasi kwamba kwa mujibu wa marehemu Sheikh Mufid (aliyefariki mwaka 413 H) katika kitabu Al-Irshad (Juzuu ya 1, uk. 175), watu wengi kutokana na ukali wa joto walikuwa wakifunga mavazi yao kwenye miguu yao.

Sibt Ibn Jawzi wa madhehebu ya Hanafi (aliyefariki mwaka 685 H) katika kitabu Tadhkirat al-Khawas (uk. 37) ameelezea kwamba waliohudhuria walikuwa watu 120,000.

Ibn Asakir ad-Dimashqi wa madhehebu ya Shafi'i (aliyefariki mwaka 571 H) katika kitabu Tarikh Dimashq (Juzuu ya 45, uk. 187) amesema kuhusu hotuba ya Mtume Mtukufu:

«فقام وقال ما شاء الله أن یقول»

"Alisimama na kusema yale ambayo Mwenyezi Mungu alitaka ayaseme."

Kauli hii inaonesha kwamba Mtume katika hali ile ya joto kali hakutoa hotuba fupi, bali aliwasilisha maudhui ndefu mbele ya mkusanyiko ule mkubwa.

Katika makala hii fupi, tunalenga kutoa baadhi ya lulu za maarifa kutoka katika hotuba hiyo ya kihistoria ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww).

Marehemu Ibn Jabr aliyefariki katika karne ya saba Hijria, katika kitabu chake cha thamani Nahj al-Iman, ameeleza khutba ya kina kuhusu hadhi na nafasi ya mtukufu huyo, na ametumia neno “Ma'ashir an-Nas” takribani mara 70, jambo ambalo ni ushahidi wa wazi kwamba; hotuba ya Mtume huyo mkubwa wa Mwenyezi Mungu ilikuwa ya kimataifa, na iliwahusu watu wote bila ubaguzi wa kundi maalumu.

1. Enyi watu: Hapa ni sehemu ya mwisho ninayosimama; basi sikilizeni, tiini, na kubalini amri ya Mola wenu, kwani Mwenyezi Mungu ni Mola wenu na Ali ni Imam wenu.

2. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Mtukuzeni Ali, kwani hakuna elimu yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu alinipa mimi, na kila alichonifundisha nimemfundisha pia Ali; yeye ndiye atakayefafanua elimu hizi kwenu baada yangu.

3. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Mtukuzeni Ali, kwani Mwenyezi Mungu amempa ubora na mkubalini kwani Mwenyezi Mungu amemteua.

4. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Ali ni Imam kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

5. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Mtukuzeni Ali, kwani yeye ndiye mbora wa watu baada yangu miongoni mwa wanaume na wanawake.

6. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Hakika Ali na watakatifu kutoka miongoni mwa watoto wangu wote wanatokana na kizazi cha Ali; wao ni Thiqal Asghar (kizito kidogo), na Qur'ani ni Thiqal Akbar (kizito kikubwa). Kauli hii ya Mtume inaashiria Hadithi sahihi na mutawatir ya Thaqalayn, ambayo imepokewa katika vyanzo vya msingi vya Ahl al-Sunnah.

7. Jueni na fahamuni kwamba mimi nimetimiza wajibu wangu, nimefikisha ujumbe ambao nilitakiwa kuwafikishia, nimeufikisha masikioni mwenu na nimewaeleza kwa uwazi. Jueni... jueni kwamba hakuna mtu mwingine isipokuwa ndugu yangu (Ali) ambaye ni Amirul-Muuminin, na uongozi juu ya watu baada yangu si halali kwa yeyote isipokuwa Ali.

8. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Huyu Ali ni ndugu yangu na khalifa wangu kwa kila anayeniamini, na Ali ndiye mfasiri wa Kitabu cha Mola.

9. Ma'ashir an-Nas: Hakika Mwenyezi Mungu ameikamilisha dini yake juu yenu kupitia Uimamu wa Ali, ni wazi kuwa kauli hii ya Mtume wa Mwenyezi Mungu inaashiria Aya isemayo:

«الیوم اکملت لکم دینکم و أتممت علیکم نعمتی و رضیت لکم الاسلام دینا»

"Leo nimekukamilishieni dini yenu, nimewatimizieni neema Yangu, na nimewaridhieni Uislamu kuwa dini yenu."

10. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Yeye (Ali) anasimamisha dini ya Mwenyezi Mungu na anamtetea Mtume wa Mwenyezi Mungu, Yeye ni msafi, mtakatifu, mwongozaji na mwenye kuongozwa, Mtume ni Nabii bora, na yeye ni wasii bora.

11. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Kizazi cha kila Nabii kinatokana na kizazi chake, na kizazi changu kinatokana na Amirul-Muuminin Ali bin Abi Talib.

12. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Nuru ya Mwenyezi Mungu ipo ndani yangu, kisha ndani ya Ali, na baada yake ipo katika kizazi chake mpaka kusimama kwa Mahdi ambaye atarejesha haki ya Mwenyezi Mungu na haki yetu.

13. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Mimi ni njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyooka ambayo Mwenyezi Mungu amewaamrisha mpitie katika njia ya uongofu, na baada yangu Ali, na baada ya Ali Maimamu wa uongofu kutoka katika kizazi chake watakuongozeni kwenye haki na uadilifu.

14. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Hakika mimi ni mwonyaji na Ali ni mtoaji wa bishara njema. Enyi watu! Mimi ni mwonyaji na Ali ni mwongozaji. Enyi watu! Mimi ni Nabii na Ali ni wasii wangu.

15. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ali ni Imam, na Maimamu baada yake ni watoto wake, na mimi ni baba wa wote hao, na wote hao wanatokana na kizazi chake, Al-Qaim Mahdi ambaye atashinda dini zote anatokana nasi.

Hakika yeye ni mwenye kulipiza kisasi kwa madhalimu, mshindi na mbomoaji wa ngome, Hakika yeye ni msaidizi wa dini ya Mwenyezi Mungu, taa katika bahari yenye kina kirefu, mrithi wa elimu zote na mjuzi wa maarifa yote... yeye ni hoja iliyobaki ya Mwenyezi Mungu na baada yake hakuna hoja nyingine, haki haipo isipokuwa pamoja naye, na nuru zote zipo kwake... Jueni kwamba yeye ni Walii wa Mwenyezi Mungu duniani.

16. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Qur'ani ipo kati yenu na Ali pamoja na Maimamu baada yake watakuwa miongoni mwenu, nami nimewatambulisha kuwa wao wanatokana nami na Ali, muda wa kuwa mtashikamana nao, hamtapotea.

17. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Fadhila za Amirul-Muuminin Ali bin Abi Talib mbele ya Mwenyezi Mungu ni nyingi sana, na Mwenyezi Mungu ameziteremsha ndani ya Qur'ani, idadi yake ni kubwa mno kiasi kwamba haiwezi kuhesabiwa katika kikao kimoja.

18. Ma'ashir an-Nas: Enyi watu: Yeyote atakayemtii Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, Ali na Maimamu wengine niliowataja, atapata mafanikio makubwa.

Lulu za Maarifa

Katika vipengele hivi 18 vya Khutba ya Ghadir, inawezekana kubainisha mihimili kadhaa, bali lulu kadhaa za maarifa, kama ifuatavyo:

1. Uashiriaji wa Wilayah, Uimamu na uhalali wa ukhalifa wa Ali (as).

2. Uashiriaji wa ubora na ujuzi wa Amirul-Muuminin (as) juu ya waliokuwepo.

3. Kila elimu aliyofundishwa Mtume na Mwenyezi Mungu, pia ilitolewa kwa Amirul-Muuminin.

4. Uazao na Ahlul-Bayt wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) wanatokana na kizazi na mti wa uzazi wa Ali (as).

5. Uashiriaji wa Hadithi sahihi na mutawatir ya Thaqalayn.

6. Kutimizwa kwa hoja (Itmam al-Hujjah) na Mtume Mtukufu kwa watu wote waliokuwepo.

7. Kukamilika kwa dini ya Mwenyezi Mungu kwa Wilayah na Uimamu wa Amirul-Muuminin Ali (as).

8. Uashiriaji wa Uimamu wa Imam wa Zama (as) na suala muhimu la Mahdawiyya.

9. Imam wa Zama (as) ni msaidizi wa dini ya Mwenyezi Mungu.

10. Imam wa Zama ni mrithi wa elimu zote.

11. Imam wa Zama ni Walii wa Mwenyezi Mungu juu ya ardhi.

12. Uokovu wa binadamu unategemea kumtii Ali (as).

13. Katika sehemu nyingi, Qur’ani Tukufu imeashiria fadhila na ubora wa Amirul-Muuminin (as).

14. Maimamu wengine wote wanatokana na Mtume wa Mwenyezi Mungu na kutoka katika kizazi cha Amirul-Muuminin Ali (as).

Mtu wa kwanza kutoa bay'ah kwa Ali (as)

Marehemu Ibn Jabr baada ya kumalizika kwa hotuba ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) na khutba ya Ghadir anasema: Mtu wa kwanza aliyeshikana mkono na Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumpa bay'ah Ali (as) alikuwa Abu Bakr, Umar, Uthman, Talha na Zubair pamoja na masahaba wengine wote miongoni Muhajirina na Ansar.

Sasa swali linalojitokeza katika fikra za wengi ni: Je, waliotoa bay'ah walitekeleza ahadi yao au waliivunja?

Hafidh Dhahabi (aliyefariki mwaka 748 H) katika kitabu Siyar A'lam an-Nubala (Juzuu 19, uk. 328) amenukuu kutoka kitabu Sirr al-‘Alamayn wa Kashf ma fi ad-Darayn cha Ghazali kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika siku ya Ghadir alisema: “Man kuntu mawlahu fa ‘Aliyyun mawlahu”, na Umar akamwambia Ali (as): “Bakhin bakh, asbahta mawlaaya wa mawla kulli mu’minin wa mu’mina”, yaani “Hongera, umekuwa kiongozi wangu na kiongozi wa kila Muislamu mwanaume na mwanamke.”

Dhahabi kisha anaandika kwamba Ghazali amesema kauli hii ya Umar ilikuwa ni kukubali na kuridhia Wilayah ya Ali, lakini tamaa ya uongozi na ukhalifa ilimshinda, mpaka wakapingana na kugeuka nyuma na kununua ukhalifa kwa thamani duni, na ni biashara mbaya waliyoifanya.

Kauli hii ya Ghazali ni dalili ya wazi ya kuvunjwa kwa bay'ah.

Mihimili 18 ya Dhahabu katika Khutba ya Ghadir

Mhakiki na mwandishi; Muhammad Ja'far Tabasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha