Jumapili 31 Mei 2026 - 12:21
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf akosoa kuibua mgawanyiko wa kimadhehebu miongoni mwa baadhi ya viongozi wa nchi za Kiarabu za Ghuba

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji amesema: “Wakati ripoti rasmi zimetangaza kuwa idadi ya mahujaji wa mwaka huu ni watu 1,700,000, ripoti za awali kuhusu ziara ya Imam Hussein (as) katika siku ya Arafah zinaonyesha kuwa idadi hiyo kwa makadirio ya awali imevuka watu 7,000,000.”

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Swala ya Ijumaa alizozitoa katika Husainiyya Kuu ya Fatimiyya, Najaf Ashraf, alisema:

“Sifa na shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu Mtukufu na Aliyetukuka, na pia kwa wananchi wetu wapendwa pamoja na taasisi zetu za kijamii na za serikali kutokana na mafanikio ya ziara ya Imam Hussein (as) katika usiku na siku ya Arafah, wakati ripoti rasmi zimetangaza kuwa idadi ya mahujaji wa mwaka huu ni watu 1,700,000, ripoti za awali kuhusu ziara ya Imam Hussein (as) zinaonyesha kuwa idadi ya mazuwari kwa makadirio ya awali imevuka watu 7,000,000, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu bila ya kutokea tatizo lolote, bado tunasubiri taarifa rasmi kuhusu suala hili,” maneno haya yalitolewa katika khutba ya Swala ya Ijumaa mjini Najaf Ashraf.

Kuhusu masuala ya kimataifa

Alizungumzia ripoti za kimataifa kuhusu watu 7,500 wa Pakistan kufanywa wakimbizi na mali zao kufungiwa kwa sababu tu ya kuwa Mashia, na akauliza:

“Viwango vya ubinadamu na haki viko wapi katika hatua kama hizi? Wakati katiba za nchi hizi zinazungumzia misingi ya usawa na uhuru wa itikadi na maoni, lakini kwa vitendo kwa kuwafukuza watu hawa kwa sababu ya kuwa Mashia, wanakuza utamaduni wa chuki.”

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf pia alirejelea mashambulizi na uvamizi wa anga wa Israel kusini mwa Lebanon ambao umepelekea kuuawa kishahidi na kujeruhiwa kwa watu kadhaa; na hayo yote yakitokea chini ya kivuli cha ukimya wa kimataifa, ilhali dunia inazungumzia kuanzishwa kwa amani.

Lakini inaonekana wito huu wa amani ni wa upande mmoja tu na unaelekezwa kwa mataifa yetu, si kwa Israel. Hapa linaibuka swali hili: “Israel iko upande gani wa amani? Umoja wa Mataifa uko wapi katika mradi wa amani? Kwa nini hauiwekei lawama Israel kwa mashambulizi haya ya mara kwa mara?”

Khutba ya kidini

Khatibu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, baada ya kusisitiza uchamungu, alikumbusha sehemu ya dua ya Imam Hussein (as) ya siku ya Arafah ambayo ndani yake imekuja: 

إلهی أنا الفقیر فی غنای فکیف لا أکون فقیراً فی فقری، وأنا الجاهل فی علمی فکیف لا أکون جهولاً فی جهلی، إلهی من کانت محاسنه مساوئَ کیف لا تکون مساوئُه مساوئَ، ومن کانت حقائقه دعاوی کیف لا تکون دعاواه دعاوی، إلهی منی ما یلیق بلؤمی ومنک ما یلیق بکرمک

"Ewe Mola wangu! Mimi ni fakiri hata katika hali yangu ya kujitosheleza, basi vipi nisiwe fakiri katika hali yangu ya uhitaji? Mola wangu! Mimi ni mjinga hata katika yale ninayoyajua, basi vipi nisiwe mjinga katika yale nisiyoyajua? Mola wangu! Mwenendo mbalimbali wa mipango Yako, mabadiliko yake, na kasi ya kutimia kwa makadirio Yako, vimewazuia wanaokujua wasitulie kwa neema zako wala wasikate tamaa na Wewe wakati wa mitihani. Mola wangu! Kutoka kwangu hutoka yale yanayofaa unyonge wangu, na kutoka Kwako hutoka yale yanayofaa ukarimu Wako.

Baadaye alitoa ufafanuzi na maelezo juu ya vipengele hivi vikubwa vya malezi.

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji alisema: “Tuko mbele ya maadhimisho ya Sikukuu ya Ghadir, na tunatarajia kuwa wiki hii iwe wiki ya Wilaya, hapa pia alirejelea hadithi ya Imam Baqir (as) iliyosema:

بُنی الإسلام علی خمس: الصلاة والصوم والزکاة والحج والولایة، وما نودی بشیء کما نودی بالولایة، لأنها مفتاحهن

"Uislamu umejengwa juu ya mambo matano: Swala, Saumu, Zaka, Hija na Wilaya; na hakuna jambo lililohimizwa kama ilivyohimizwa Wilaya, kwa sababu Wilaya ndiyo ufunguo wa mambo hayo yote".

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha