Jumanne 26 Mei 2026 - 15:00
Wawakilishi wa Iran washiriki katika Foram ya Kazan 2026 nchini Urusi

Hawza/ Wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pembezoni mwa Kongamano la “Urusi – Ulimwengu wa Kiislamu: Forum ya Kazan 2026”, walishiriki katika mazungumzo na wenzao wa Urusi kuhusu ushirikiano wa kitamaduni.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walishiriki pembezoni mwa Kongamano la “Urusi – Ulimwengu wa Kiislamu: KazanForum 2026” walishiriki katika mazungumzo na wenzao wa Urusi kuhusu njia za kuendeleza ushirikiano wa kitamaduni.

Katika muktadha huo, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Mohammad Mahdi Imanipour, Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran, alikutana na Olga Lyubimova, Waziri wa Utamaduni wa Urusi, na kufanya mazungumzo kuhusu kupanua ushirikiano wa pande mbili, ikiwa ni pamoja na kuandaa Wiki ya Utamaduni wa Iran nchini Urusi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Urusi, Imanipour katika mkutano huo aliushukuru upande wa Urusi kwa mwaliko na ukarimu wao, aidha, alitoa shukrani kwa msaada wa Shirikisho la Urusi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mazingira ya vita, na akasisitiza nafasi ya kujenga na yenye ushawishi ya Urusi katika maendeleo ya ulimwengu wa Kiislamu.

Mkuu huyo wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu alisisitiza umuhimu wa kuhuisha kamati ya pamoja ya kitamaduni kati ya Iran na Urusi, na akatangaza utayari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuandaa Wiki ya Utamaduni wa Iran nchini Urusi mwezi Septemba, kwa mujibu wake, sehemu ya programu hizo inaweza kufanyika katika mji wa Kazan, ambao umechaguliwa kuwa mji mkuu wa kitamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu kwa mwaka 2026.

Mwisho wa hotuba yake, alisisitiza nafasi muhimu ya wanadiplomasia katika kuimarisha mahusiano ya kitamaduni na akaeleza kuwa; watengenezaji wa filamu wa Iran wako tayari kushiriki katika tamasha mbalimbali za filamu nchini Urusi.

Waziri wa Utamaduni wa Urusi naye alitoa shukrani kwa ujumbe wa Iran kwa kushiriki katika KazanForum 2026, pia alizungumzia mafanikio ya Wiki ya Utamaduni wa Urusi nchini Iran, na akamkaribisha Majid Majidi kushiriki katika tukio la hivi karibuni la kitamaduni nchini Urusi pamoja na kuonyeshwa kwa filamu ya Iran iitwayo Khodaye Jang (Mungu wa Vita).

Lyubimova pia alisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa filamu kati ya nchi hizo mbili, ikiwemo mpango wa kuonyeshwa kwa filamu ya Kirusi “Mtoto” nchini Iran, na akakumbusha umuhimu wa kuimarisha makubaliano katika nyanja za sinema na sanaa.

Mwishoni mwa mkutano huo, Waziri wa Utamaduni wa Urusi aliualika ujumbe wa Iran kushiriki katika Tamasha la "Intermuseum Festival" mwezi Mei pamoja na Kongamano la Utamaduni la "Saint Petersburg" mwezi Septemba. Pia alieleza matumaini yake kwamba ujumbe wa Iran pamoja na watoto wa Iran watakuwa na ushiriki mkubwa katika tamasha la utamaduni na watoto nchini Urusi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la IRNA, Kazem Jalali, Balozi wa Iran nchini Urusi, ambaye alihudhuria mazungumzo kati ya Lyubimova na Imanipour, alitoa hotuba ndani ya mfumo wa Kongamano la Kazan kuhusu hali ya sasa ya mahusiano ya pande mbili na nafasi ya mazungumzo ya kitamaduni katika jiografia ya kisiasa ya kisasa.

Kwa mtazamo wa Jalali, mabadilishano ya kitamaduni ni nyenzo yenye nguvu katika kukabiliana na mashinikizo ya kiitikadi, na kwamba mawasiliano kati ya mataifa ndiyo njia bora zaidi ya kushinda dhana za “ubora wa kitamaduni” ambazo baadhi ya nchi za Magharibi zinajaribu kuwapatia wengine.

Pia alisisitiza kwamba; Tehran inaona juhudi za baadhi ya serikali na mikondo ya kisiasa za kuwasilisha tamaduni zao kama zilizo bora kuliko za wengine kuwa jambo lisilo sahihi kimsingi.

Mwanadiplomasia huyo alieleza: "Ushirikiano kati ya Tehran na Moscow leo umeingia rasmi katika hatua ya kimkakati, tunaona uwezo mkubwa sana wa kupanua zaidi mahusiano katika nyanja mbalimbali."

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha