Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Asadullah Badamchian, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chama cha Kiislamu cha Mu’talifa, katika mazungumzo na Shirika la Habari la Hawza, akirejelea safari ya hivi karibuni ya Donald Trump kwenda China, aliitaja safari hiyo kuwa ni kosa kubwa kwake.
Alisema: China ni mpinzani wa Marekani katika medani ya kimataifa, na Trump anataka Marekani iwe ya kwanza duniani, lakini safari hii imekumbusha nguvu ya China na udhaifu wa Marekani, China ina azma kubwa ya kuiona Marekani ikidorora katika uwanja wa kimataifa, na walimwengu wanalijua hilo, safari ya Trump imeonesha nafasi dhaifu na ya chini ya Marekani, na ilikuwa ni sehemu kubwa ya udhaifu kwa Marekani.
Badamchian aliendelea kusema: Safari hii imefanyika katika mazingira ambayo uvamizi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran mwaka 1404 H.Sh., katika Vita vya Ramadhani, ulipelekea kuongezeka kwa nguvu ya Iran, na Marekani pamoja na utawala huo vamizi wameshindwa kufikia malengo yao mbele ya Iran. Kutokana na hali hiyo, Mlango wa Hormuz umeingia chini ya udhibiti wa Iran, na mzingiro wa Marekani pamoja na mayowe ya Trump ya kusema “fungueni mlango huu uliolaaniwa” hayajakuwa na athari yoyote, nchi ambazo hadi jana zilikuwa zikijizuia kufanya ushirikiano wa kiuchumi na Iran kwa kuzingatia Marekani, sasa zinaambatana na Iran ili meli zinazopita katika njia zao ziweze kufika salama katika malengo yao.
Alisema: Katika mazingira kama haya, mkutano wa Trump na viongozi wa China umeweka wazi zaidi hali dhaifu na isiyofaa ya Marekani, jambo ambalo lilikuwa kwa manufaa ya China na litakuwa na madhara mabaya kwa Marekani, taswira iliyopo duniani ni kwamba; Marekani imeshindwa kufungua Mlango wa Hormuz na hata mzingiro wake wa baharini umeshindwa licha ya gharama kubwa, hivyo inaelekea China ili kuiomba izungumze na Iran kuhusu kufunguliwa kwa Mlango wa Hormuz, hili lina maana ya udhaifu na fedheha kwa Marekani pamoja na nguvu kuu ya China na Iran.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chama cha Mu’talifa aliendelea kusema: China katika siasa za kimataifa inaambatana na Iran, na ina uadui na Marekani kuhusu Taiwan, katika hali hiyo, Iran inaambatana na China kuhusu suala la Taiwan na hushirikiana nayo katika majukwaa ya kimataifa, ilhali Marekani huipatia Taiwan silaha, hata mtu wa kawaida anaelewa kwamba China haiwezi kuambatana na Marekani katika uadui wake dhidi ya Iran, jambo ambalo lilionekana pia katika safari hii.
Akiashiria kwamba mazungumzo kati ya Xi na Trump pia yamezaa matokeo hasi kwa Marekani, aliendelea kusema: Mahojiano ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China yalisisitiza kutokuwa na manufaa kwa safari hiyo, video ya safari ya Trump ambayo Ikulu ya White House imeitoa pamoja na picha za vyombo vya habari vya dunia, inamuonyesha kiongozi wa China akiwa imara huku akitabasamu kwa ushindi, ilhali Trump hana hali kama hiyo, hali hizi mbili zinaonyesha ushindi wa kiongozi wa China katika safari hii na kudhihirisha kuporomoka kwa hadhi ya Marekani, kujipendekeza na kumsifu Trump kiongozi wa China pia ni ushahidi mwingine wa safari hii iliyojaa kushindwa na fedheha.
Badamchian alisisitiza: Trump katika safari yake ya China amefanya makosa mengi; miongoni mwa hayo ni juhudi za kulegeza uhusiano kati ya China na Iran, hili lilikuwa kosa lake, kwa sababu China ni nguvu yenye ushawishi mkubwa zaidi kuliko Marekani, na ina ushawishi katika eneo la Asia Magharibi na miongoni mwa Waislamu, na ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa wa China na Iran uko katika kiwango cha juu, suala la Mlango wa Hormuz pia limeongeza umuhimu wa mahusiano ya China na Iran.
Aliendelea kusema: China haitapunguza kamwe uhusiano wake na Iran kwa manufaa ya Trump, Trump alikuwa amemtaka Xi asinunue mafuta Iran na badala yake anunue kutoka Marekani, lakini alikataliwa, suala hili lilikuwa dhidi ya tawala ya Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani pia alitangaza akiwa China kwamba “hatuhitajii China kuhusu Mlango wa Hormuz na mafuta,” ili kupunguza mvutano wa mazingira yaliyopo.
Badamchian alisema: Kosa jingine la Trump linahusiana na Mlango wa Hormuz; China haina tatizo lolote na Iran katika Mlango wa Hormuz na Bab al-Mandab, bali Iran pia inaambatana na China katika mazingira hayo, Trump kwa kuibua suala hili ameisababishia yeye mwenyewe Marekani madhara makubwa, kosa lake jingine ni kwamba anataka kuiangamiza Iran na kuirudisha katika zama za mawe, ilhali China inapinga kabisa sera hiyo, Trump alidhani angeweza kutumia chuki dhidi ya Iran akiwa China kwa manufaa yake.
Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Chama cha Mu’talifa aliendelea kusema: Iran imekuwa ikitumia na itaendelea kutumia kosa hili la Trump katika kuinua uhusiano wake na China, Bwana Araghchi katika mkutano wa BRICS nchini India ametumia vizuri mahusiano hayo pamoja na China, Urusi na India, na amefanya mazungumzo mazuri.
Badamchian aliongeza: Kushindwa kwa Trump katika safari ya China kutazifanya nchi nyingine zizingatie nguvu ya Iran kuwa dola ya kimataifa na kupuuza vitisho vya Marekani, safari hii imekuwa na manufaa zaidi kwa China na Iran na hasara kwa Marekani.
Mwisho alisema: Trump angeweza kufaidika na safari ya China na badala ya kutoa madai yasiyokubalika, angeweza kuibua masuala ambayo China ingemtaka ayatekeleze, kama kusitisha vita dhidi ya Iran au kuondoa mzingiro wa baharini, lakini kutokana na kiburi chake cha kifirauni, hakufaulu kutumia fursa hiyo, mustakabali wa Marekani utaendelea kuwa wa giza ikiwa mwenendo huu utaendelea, na wananchi wa Marekani wana haki ya kupaza zaidi kaulimbiu ya “Hapana kwa ufalme.”
Maoni yako