Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Kamati ya “Hatua kwa ajili ya Palestina” kupitia taarifa yake ilipinga uwepo wa kampuni za kimataifa zinazojishughulisha na viwanda vya kijeshi katika maonesho ya SAHA 2026 mjini Istanbul, na kuzitaja kampuni hizo kuwa ni “washirika wa kimkakati wa jinai na mauaji ya kimbari nchini Palestina.”
Maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa udhamini wa Rais wa Uturuki katika Kituo cha Maonesho cha Istanbul, yanahusisha kampuni mbalimbali zikiwemo BAE Systems, L3Harris, Leonardo, Airbus, Siemens na Thales UK; kampuni ambazo zina nafasi katika usambazaji wa silaha, vipuri vya kijeshi na teknolojia zinazotumiwa na jeshi la Israel.
Kamati ya Hatua kwa ajili ya Palestina katika taarifa yake ilisema: “Kampuni hizi zimepata fursa ya kuuza silaha na teknolojia zinazotumika dhidi ya wananchi wa Palestina mjini Istanbul.”
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kampuni ya L3Harris ndiyo inayosambaza mifumo ya kielektroniki ya ndege za kivita za F-35 za Israel, na BAE Systems pia inatoa vipuri vya ndege za kivita, risasi, mifumo ya kurusha makombora na magari ya kivita kwa jeshi la Israel.
Kamati hiyo pia ilitangaza kwamba; kampuni ya Airbus inashiriki katika utengenezaji wa droni zinazotumiwa na Israel, huku kampuni za Siemens na Thales UK nazo zikitoa huduma na vifaa vya kiufundi vinavyohusiana na viwanda vya kijeshi vya Israel.
Inafaa kutajwa kwamba Kamati ya Hatua kwa ajili ya Palestina, ambayo iliundwa mwaka 2024 sambamba na kumbukumbu ya miaka 76 ya “Nakba” ya Palestina kwa ushiriki wa makumi ya taasisi za kisiasa, vyama na mashirika ya kitaaluma nchini Uturuki, imetangaza kwamba; lengo lake ni kuunda “mstari wa mshikamano wa kimsingi na Palestina” na kujitahidi kukata kabisa mahusiano na Israel.

Maoni yako