Jumatatu 11 Mei 2026 - 07:00
Wanajeshi wa Kizayuni waendeleza tabia yao ya kutoheshimu vitakatifu vya Wakristo kusini mwa Lebanon

Hawza/ Kudhalilishwa kwa matakatifu ya Wakristo na askari wa Kizayuni nchini Lebanon; kuanzia kuvunja sanamu ya Nabii Isa (as) hadi kuweka sigara mdomoni mwa sanamu ya Bibi Maryam (as).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari ikiwemo tovuti ya “Kurekodi Mauaji ya Kimbari ya Israel”, mwanajeshi mmoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni wakati wa mashambulizi dhidi ya kusini mwa Lebanon, ameonesha dharau kwa kuweka sigara mdomoni mwa sanamu ya Bibi Maryam (as).

Hatua hii ya aibu imefanyika katika kijiji cha Wakristo kiitwacho “Dibl”. Takribani mwezi mmoja uliopita pia picha kutoka eneo hilo hilo zilichapishwa zikionesha askari mmoja wa Israel akivunja kichwa cha sanamu ya Nabii Isa (as) kwa kutumia nyundo kubwa.

Jeshi la Israel lililazimika kuwakamata na kuwafukuza kwa njia ya maonyesho askari wake wawili baada ya wimbi kubwa la lawama na ukosoaji wa kimataifa, lakini hatua hii mpya ya kulidhalilisha sanamu ya Bibi Maryam (as) inathibitisha kwamba mwenendo huu umeota mizizi miongoni mwa wanajeshi wa Kizayuni, na hata adhabu za kulazimishwa na za juu juu hazijaweza kuzuia kurudiwa kwa kuvunjiwa heshima matakatifu hayo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha