Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kikao cha pili cha kimataifa cha kielimu chenye anuani “Daraja kati ya walimwengu, kujenga amani” kilifanyika siku ya Alhamisi, tarehe 30 April 2026, kwa juhudi za Ofisi ya Dini na Madhehebu ya Naibu wa Mawasiliano na Masuala ya Kimataifa ya Hawza, kwa ushirikiano na Taasisi ya Kielimu na Utafiti ya Imam Khomeini (Rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), Jamiat al-Zahra, pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Vatican.
Katika kikao hicho, Profesa “Andrea Bisogero”, mwalimu wa historia na falsafa ya kisasa na ya zama za sasa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum nchini Italia, huku akirejelea kwamba; dini wakati mwingine imegeuzwa kuwa chombo cha kuhalalisha vita na tamaa ya madaraka, alisisitiza umuhimu wa kufanya mapitio upya ya ufanisi wa dini katika zama za sasa.
Maoni yako