Jumapili 3 Mei 2026 - 17:30
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Tanzania wamepokea nakala ya wasifu wa Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (ra)

Hawza/ katika hatua inayolenga kukuza uelewa wa kihistoria na kielimu kuhusu maisha ya viongozi wa Kiislamu waliotoa mchango mkubwa katika harakati za kisiasa na kijamii, wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Tanzania wamepokea nakala ya wasifu wa Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei(ra), Kitabu hicho kinachukua nafasi muhimu kama rejea ya kipekee, huku kikitoa mwanga juu ya maisha ya kiongozi huyo kupitia simulizi zake binafsi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katika maudhui yake, kitabu hicho kinaelezea kwa kina vipindi mbalimbali vya maisha ya kiongozi huyo wa kiroho, vikiwemo nyakati za kifungo, uhamisho wa kulazimishwa, pamoja na mateso aliyokumbana nayo wakati wa utawala wa Pahlavi nchini Iran. Simulizi hizi zinatoa taswira halisi ya mapambano aliyoyapitia, na jinsi alivyosimama kidete katika kulinda misingi ya itikadi na haki za jamii.

Aidha, wanafunzi waliopokea nakala hizo wameeleza kuwa kitabu hicho kina thamani kubwa kielimu na kihistoria, kwani kinawapa fursa ya kujifunza moja kwa moja kutoka kwa ushuhuda wa mhusika mwenyewe. Kupitia simulizi hizo, wasomaji wanaweza kuelewa kwa undani zaidi mazingira ya kisiasa ya wakati huo na nafasi ya harakati za mapambano katika kuleta mabadiliko ya kijamii.

Toleo la awali la kitabu hiki liliandaliwa kwa lugha ya Kiarabu na Dkt. Mohammad Ali Azarshab na kuchapishwa mjini Beirut. Toleo hilo linahesabika kuwa ushuhuda muhimu wa kihistoria, likiwa limejengwa juu ya simulizi za moja kwa moja kutoka kwa mhusika, jambo linaloongeza uhalisia na uzito wa maudhui yake katika nyanja za utafiti na elimu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha