Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Abdullah Gül, rais wa kumi na moja wa Uturuki ambaye alishiriki katika “Jukwaa la Kiuchumi la Delphi” nchini Ugiriki, akizungumzia vita ndani ya Asia Magharibi alisema kwamba; katika mchakato huu sura ya Marekani imeathirika, na nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi pia zimepoteza imani yao kuhusu nguvu ya Marekani.
Aidha aliitaja Israel kuwa ndiyo inayowajibika kwa mateso na machungu yaliyopo katika eneo hilo, na akasema: Dunia inapitia kipindi cha mgogoro wa kimataifa na kutokuwa na utulivu, ambapo baadhi ya serikali zenye nguvu zimeidhoofisha mfumo unaotegemea kanuni na desturi za kimataifa.
Akiashiria kwamba mashambulizi dhidi ya Ghaza, Iran na Lebanon yamekuwa ya uharibifu mkubwa, alisema: “Operesheni hizi zimepuuza kanuni za kimataifa, zimesababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Kwa mujibu wa maoni ya wataalamu na ripoti za Umoja wa Mataifa, hali ya Ghaza imegeuka kuwa mauaji ya kimbari.”
Gül akisisitiza kwamba; mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran pia yatakuwa na athari za kimkakati kwa muda mrefu katika ngazi ya kikanda na kimataifa, alisema: “Hata maafisa wa Marekani wanakiri kwamba Tehran si tishio la haraka kwa Marekani. Marekani kwa mwenendo huu inafungua njia kwa hatua zisizo halali za madola mengine pia.”
Aidha, alisisitiza tena kwamba katika mchakato huu sura ya Marekani imeathirika na nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi pia zimepoteza imani yao kwa nguvu ya Marekani.
Rais huyo wa zamani wa Uturuki, huku akirejea kwamba Mlango-Bahari wa Hormuz umegeuka kuwa changamoto mpya aliongeza kuwa; usambazaji wa nishati duniani pia umeathirika vibaya.
Akiashiria kwamba Israel imetengwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote, alisema: “Israel ndiyo inayowajibika kwa mateso yaliyopo katika eneo hilo. Maadamu sera zinazoitwa za eneo la buffer (ukanda wa magharibi), uvamizi na ujenzi haramu wa makazi dhidi ya nchi jirani zitaendelea, hali hasi katika eneo hilo haitabadilika.”
Maoni yako