Jumamosi 18 Aprili 2026 - 15:30
Ukosoaji mpya wa Papa dhidi ya Trump na Netanyahu: Dunia inaharibiwa mikononi mwa  madikteta wachache

Hawza/ Kufuatia matamshi ya hivi karibuni ya Donald Trump kuhusu vita dhidi ya Iran na kuongezeka kwa mvutano kutoka Washington na Tel Aviv, Papa amewalaani viongozi wanaotumia dini vibaya ili kuhalalisha vita na kusisitiza kuwa; kundi dogo la madikteta linaendelea kuiharibu dunia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kiongozi wa Kanisa Katoliki, baada ya mashambulizi ya maneno ya mara kwa mara yaliyofanywa na Donald Trump dhidi ya misimamo yake kuhusu vita na Iran, alisisitiza kwa uthabiti: “Dunia inaharibiwa mikononi mwa madikteta wachache.”

Kauli hizi wazi zilitolewa na Pope Leo XIV katika hotuba yake ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph mjini Bamenda, kaskazini-magharibi mwa Cameroon, katika muktadha wa ziara yake ya kihistoria katika nchi nne za Afrika.

Alisema: “Ole wao wanaotumia dini na hata jina la Mungu kwa maslahi yao ya kijeshi, kiuchumi na kisiasa, na kuvuta vitu vitakatifu katika giza na uchafu.”

Kwa mtazamo huu, Papa ambaye ni mkosoaji wa uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, kwa mara nyingine alilaani kwa uwazi zaidi viongozi wanaotumia lugha ya kidini kuhalalisha uvamizi wa kijeshi. Waziri wa ulinzi wa Marekani hapo awali alikuwa amesema kuwa wanajeshi wa Marekani “wanapigana kwa ajili ya Yesu.”

Papa aliendelea kusema: “Dunia inaharibiwa mikononi mwa wachache madikteta, lakini kinachoifanya ibaki imara ni umati mkubwa wa ndugu na dada wenye mshikamano.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha