Jumamosi 18 Aprili 2026 - 14:30
Upanuzi wa shughuli za kielimu za Taasisi ya Haram Tukufu ya Imamu Husein (as) barani Afrika

Hawza/ Taasisi ya masuala ya kitamaduni ya Haram ya Imamu Husayn (as) inaendelea kwa nguvu shughuli zake za kielimu na kitamaduni katika Afrika Magharibi.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Abdulghaffar Al-Maliki, Mkurugenzi wa masuala ya Afrika katika Taasisi ya Kitamaduni ya Haram ya Imamu Hussein (as), katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti rasmi ya taasisi hiyo alisema: Kitengo cha shughuli za Haram katika uwanja wa Afrika, kilicho chini ya Idara ya Masuala ya Kidini ya Haram Tukufu ya Imamu Husayn (as), kinaendelea kwa nguvu kutekeleza programu zake za kielimu na kiibada katika nchi za Afrika Magharibi. Programu hizi zinajumuisha kuandaa kozi za masomo ya kina ambazo makundi mbalimbali ya jamii, hususan vijana huko Nigeria, Niger na Guinea, wanaweza kushiriki.

Aliongeza kuwa: “Kozi hizi za kielimu zimejikita katika mada za kiitikadi, kifiqhi na kimaadili, hasa misingi ya dini na Tawhidi, masuala ya Ijtihadi na Taqlidi, pamoja na hukumu za twahara. Aidha, pia zimepangwa masomo ya vitendo kwa watoto kuhusu namna sahihi ya kutawadha, kwa lengo la kupandikiza hukumu za dini kwa njia ya vitendo ndani ya jamii.”

Chanzo: imamhussain.org

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha