Jumapili 12 Aprili 2026 - 21:30
Neno la Walii | Tawfiki ya kushukuru: Neema kubwa katika mtazamo wa Qur’ani

Hawza/ Katika sehemu hii ya maelezo, imeashiriwa maana ya ibara ya Qur’ani «أَوْزِعْنِی» ambayo ina maana ya ilhamu na tawfiki ya kivitendo kwa ajili ya kushukuru. Kushukuru neema si tu kulipa deni, bali ni njia ya kuvutia neema zaidi za Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, kiongozi mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika sehemu ya kauli zake amefafanua kuhusu tawfiki ya kushukuru katika aya za Qur’ani, ambayo tunaiwasilisha kwenu wasomi.

«رَبِّ أَوْزِعْنِی أَنْ أَشْکُرَ نِعْمَتَکَ الَّتِی أَنْعَمْتَ عَلَیَّ وَ عَلَیٰ وَالِدَیَّ»


 — «أَوْزِعْنِی» ina maana kwamba inaweza kusemwa: “Nipe ilhamu.” Na bila shaka ilhamu hii ni ya kivitendo, inaweza kusemwa: “Nipe tawfiki.”

«اَن اَشکُرَ نِعمَتَکَ الَّتی اَنعَمتَ عَلَیَّ» —

kwamba niweze kushukuru neema ile uliyonijalia. «وَ عَلی والِدَیَّ» — na neema ile uliyojalia wazazi wangu niweze kuishukuru.

Shukrani yenyewe si kwamba mtu anarejesha deni lake tu; bali shukrani yenyewe bila shaka ni njia ya kuvutia neema nyingi zaidi. Ikiwa mtu kila siku anakumbuka moja baada ya nyingine neema mbalimbali za Mwenyezi Mungu na kuzishukuru, na hasa ikiwa hali hiyo iko moyoni — yaani mtu kweli anahisi shukrani katika wakati huo — na kisha ulimi uoneshe au hata usioneshe, jambo hili lina athari kubwa sana na ni miongoni mwa adhkari za juu kabisa.

Kwa mtazamo wangu mnyonge, hii ni miongoni mwa matendo ya juu kabisa. Pale iliposemwa «وَ عَلی والِدَیَّ», dhahiri yake ni kwamba kila kitu kilichotolewa kwa wazazi wangu, nami nikishukuru hiyo ni hatua ya shukrani. Na kwa mtazamo wangu mdogo, sisi tukiziangalia neema zetu — ambazo ya kwanza ni uwepo wetu, kwamba tumeumbwa, katika zama hizi na mahali hapa — hili lina hesabu yake. Yaani sisi tumehesabiwa hadi tukazaliwa, tukapewa neema ya uwepo, na kisha tukapewa mpango; jambo hili ni muhimu sana.

Kwa mfano, kama utajua kwamba; Agha Muhammad Khan Qajar — hata kama humpendi — angalia kwamba aliandika jina lako katika waraka kwamba: “Mtu huyu ikiwa ningali hai nitamtuma kusoma Chuo Kikuu cha Oxford,” hata kama yeye alikufa miaka 200 iliyopita. Utahisi fahari ya kipekee. Ajabu ni kiasi gani utahisi fahari. Sasa mtu aliye juu kabisa ulimwenguni ameweka mpango huu kwa ajili yako, hali ya kuwa hana hata haja nao. Hivyo basi mwanadamu atafakari. Mtazamo mmoja tu unatosha kuelewa. Hili lenyewe ni shukrani.

Miongoni mwa mambo haya ni kushukuru uwepo wa Imamu (as), uwepo wa Ma’sum (as), na hata kushukuru Qur’ani — kwamba sisi tuwe miongoni mwa watu wa tawallaa — hata kama hatubadiliki kabisa — yenyewe tu kukutana na haya, shukrani yake ni ya juu sana.

Baadhi ya watu hujivunia kwamba walipita mara moja katika barabara fulani ngumu na ya vumbi, au walimuona mtu fulani kwa mbali, kisha kizazi kinachofuata kinasema: “Ndiyo, fulani alimuona mtu fulani alipokuwa akipita mahali fulani.” Hapana, umeelewa? Sisi kukutana kwetu na zama hizi, mahali hapa, Qur’ani Tukufu, na Ma’sum (as) — ikiwa mtu atatafakari vizuri, hata na Mwenyezi Mungu mwenyewe — lakini hilo linahitaji neema maalumu zaidi.

Na neema walizopewa wao — hasa kwa kuwa uhusiano wa Imamu (as) na sisi ni kama uhusiano wa baba — na ule upande wa huruma na mapenzi waliyonayo kwetu, wanazingatia kwa undani kabisa maslahi yetu, zaidi hata ya tunavyotamani sisi wenyewe au akili yetu kufikia.

Na kwa hiyo, ikiwa tutaelewa hata kiasi kidogo cha jambo hili — kwamba tunashughulika na nani — basi shukrani ya uwepo wake yenyewe, na vile alivyopewa, yote hayo yanapaswa kushukuriwa.

Hivyo basi, hii «وَ عَلی والِدَیَّ» — ukiiangalia — haijaishia kwa wazazi tu, bali iko juu zaidi ya hapo. Hapa tunajua kwamb;a Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) alifurahi sana kwa kuzaliwa kwa Bibi Fatima (as). Ikiwa kweli sisi tunafuatana naye, tunapaswa kufurahi kwa kiwango hicho kadiri ya uwezo wetu, na kwa hakika tushukuru: “Umempa Mtume wetu jambo kama hili” — na kadhalika hadi mwisho.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha