Jumatano 1 Aprili 2026 - 19:20
Jibu thabiti la Iran na mapigo ya Muqawama vimefichua udhaifu wa kambi za Marekani

Hawza/ Katibu Mkuu wa Muqawama wa Kiislamu “Kataib Sayyid al-Shuhadaa” huku akiisifu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ustahimilivu wake mbele ya wavamizi, alitangaza kuwa; jibu la kushtukiza la Iran na operesheni za mhimili wa Muqawama katika eneo, vimedhihirisha kwamba; kambi za Marekani zina kiwango kikubwa cha udhaifu na hazina uwezo wa kuwahakikishia usalama wengine.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Abu Alaa al-Walā’ī, Katibu Mkuu wa Muqawama wa Kiislamu “Kataib Sayyid al-Shuhadaa”, katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa X, huku akiisifu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na jibu lake lenye nguvu na la kushtukiza kwa wavamizi, alisema kuwa; jibu hili limekuwa juu zaidi ya matarajio yote ya upande wa pili.

Akiashiria baadhi ya operesheni na mapigo yaliyotolewa dhidi ya malengo ya adui, aliongeza kuwa: Hatua hizi, ikiwa ni pamoja na kulengwa kwa kiwanda cha kemikali huko Be’er al-Saba’, zinaonesha kiwango cha juu cha uwezo na usahihi katika operesheni za mhimili wa Muqawama. Al-Walā’ī pia alitoa shukrani kwa juhudi na kujitolea kwa vikosi vya mhimili wa Muqawama katika nchi mbalimbali chini ya majina tofauti.

Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhadaa aliendelea kusema: Mapigo yenye athari yaliyotolewa na vikosi vya Muqawama katika eneo lote, hasa katika ukanda wa Ghuba ya Uajemi, dhidi ya kambi za Marekani, yamefichua ukweli muhimu kwenye nchi zinazohifadhi takriban kambi 750 za kijeshi za Marekani duniani; kwamba kambi hizi zina udhaifu mkubwa na hata hazina uwezo wa kujilinda zenyewe, sembuse kuwa na uwezo wa kuhakikisha usalama wa wengine.

Aidha, akirejelea maendeleo ya hivi karibuni katika Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain, alisema: Kinachotokea katika nchi hizi kinaonesha kwamba; ukaribu uliopitiliza na sera za Marekani haujaweza kuwaletea usalama wa kweli.

Al-Walā’ī pia katika sehemu nyingine ya mazungumzo yake, huku akirejelea baadhi ya kauli za hivi karibuni za Donald Trump kumhusu Muhammad bin Salman, alisema: Kauli hizi zinaonesha kwamba; kuitegemea Marekani kupita kiasi siyo tu kwamba si dhamana ya usalama, bali kunaweza pia kusababisha kudhoofika kwa mamlaka na maslahi ya kitaifa ya nchi.

Jibu thabiti la Iran na mapigo ya Muqawama vimefichua udhaifu wa kambi za Marekani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha