Ijumaa 20 Machi 2026 - 18:10
Uchaguzi wa Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei unaashiria kuendelea kwa njia ya Muqa'wama

Hawza/ Sheikh Muhammad al-Bayati, mtafiti wa Kiislamu kutoka Iraq, amesisitiza kuwa; uteuzi wa Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei kama kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu umeleta amani katika jamii na upande wa mapinduzi, na unaashiria kuendelea kwa njia ya Muqa'wama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Muhammad al-Bayati, mtafiti wa Kiislamu kutoka Iraq, katika kongamano la pili la kimataifa "Shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei; Imam wa umoja, mlinganiaji wa Quds na Shahidi wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani," lililoandaliwa siku ya (Jumatano) na Jumuiya ya kukurubisha umoja wa dini za Kiislamu, alisisitiza kuwa; Shahidi wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Ayatollah Ali Khamenei (ra), kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alikuwa kiongozi wa umoja na mtetezi wa uhuru wa Quds, na aliishi kwa miongo kadhaa akijitolea kwenye suala la Palestina na haki za umma wa Kiislamu. Alikuwa daima akitetea kwa nguvu suala la Palestina na haki za watu wa eneo hilo katika kujitawala na kupata uhuru wao.

Aliongeza kuwa; kifo cha Imam Khamenei ni msiba mkubwa kwa umma wa Kiislamu, lakini jambo hili halitasababisha kupungua kwa ari na dhamira yetu ya kuendelea na mapambano yetu na kukamilisha jukumu letu la kuikomboa Quds na Palestina. Kama vile babu yake, Imam Hussein (a.s), alivyopata shahada kwa ajili ya kuihifadhi dini; na alikuwa daima akiwa na matumaini ya shahada.

Sheikh al-Bayati alikumbusha kwamba; shada ya Imam Khamenei itachangia zaidi umoja katika umma wa Kiislamu na itakuwa ni chombo cha kuimarisha muqawama na kuongeza dhamira ya mataifa huru katika kupinga dhuluma na uonevu.

Mtafiti huyu wa Kiiraq alisema kuwa; uteuzi wa Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei kuwa kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, baada ya kikao cha Baraza la Wanazuoni wa Kidini kwa kufuata Katiba, kumesababisha amani na utulivu katika jamii na upande wa mapinduzi. Uchaguzi wake unaashiria kuendelea kwa muqawama.

Alisisitiza kuw;a Ayatollah Sayyid Mujtaba Khamenei ataipeleka kwa nguvu meli ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuleta ustawi na maendeleo kwa Iran.

Sheikh al-Bayati aliongeza kusema kuwa, Quds mwishowe itakombolewa na Palestina itarudi kwa wamiliki wake halali.

Alisema kuwa; umoja na upinzani ndio kiungo muhimu cha kufikia ushindi na uhuru, na alisisitiza kuwa, Quds daima itakuwa ni ishara ya umoja wa Kiislamu, na kila mmoja wetu ana jukumu la kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kuikomboa kutoka katika utawala wa kivamizi wa Israeli.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha