Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah A'rafii Mkurugenzi wa hawza za kieleimu nchini Iran, katika ujumbe wake kutokana na kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei ametoa salamu za pongezi, matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحيم
Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei (zidumu baraka zake).
Nikiwa natola salamu za rambirambi kwa mara nyengine kutokana na shahada ya Kiongozi wa Mapinduzi, natoa pongezi kutokana na kuchaguliwa kwako na Baraza la wataalamu wa Uongozi. Ni matumaini yangu Taifa tukufu la Irani litachukua kiaga na kumtii Walii Faqih, kama ilivyo kuwa zama za Imaam Khomein (ra) na Imaam Shahidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na vilevile hawza za kielimu na wanazuoni wa hawza, pamoja na wanazuoni wa vyuo vikuu wataungana pamoja katika njia hii iliyojaa msaada wa Mtukufu Imaam wa Zama (ajtf).
Masiku ya utukufu na taufiki yenye kuendelea yawe nawe.
A'rafii
Mkurugenzi wa hawza nchini Iran
18/12/1404 - 9/3/2026.
Maoni yako