Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katibu wa Baraza la wataalamu wa uongozi katika maelezo yake alitangaza kuwa: Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu ameainishwa na Baraza la wataalamu wa uongozi.
بسم الله الرحمن الرحيم
Taifa tukufu na huru la Iran, amani ya Mola iwe nanyi:
Baraza la wataalamu wa uongozi, likiwa linatoa salamu za rambi rambi kutokana na shahada ya Kiongozi mtukufu Ayatullah Imaam Khamenei (ra), mashahidi wengine watukufu hasa viongozi wakuu wa vikosi vya jeshi na wanafunzi wa shule ya "Shajara Twayyibah" katika Mkoa wa M'inab, na linalaani uvamizi wa kuhofisha uliofanywa na Marekani mfanya jinai pamoja na utawala khabithi wa Wazayuni.
Tunawafahamisha kwamba, Baraza hili punde kidogo tu baada ya kuchapishwa habari za kupata shahada Kiongozi mwenye hekima wa Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na masharti mazito ya vita na vitisho vya moja kwa moja kutoka kwa maadui kuwaelekea watu wa Irani, na kulipua ofisi za katibu wa Baraza la wataalamu wa uongozi, milipuko ambayo ilisababisha baadhi ya wafanyakazi na timu ya walinzi kupata shahada.
Baraza hili kwa mujibu wa katiba na muongozo wa ndani ya Baraza la wataalamu wa uongozi, zilifuatwa taratibu maalumu kwa ajili ya kuweza kufanyika vikao vitakavyo wezesha upatikanaji wa Kiongozi mpya wa Mapinduzi.
Baraza la wataalamu wa uongozi, kutokana na faida ya nafasi ya juu ya wilayat faqih katika kipindi cha ghaiba ya Imaam wa Zama (ajf), na kutilia umuhimu mas-ala ya Kiongozi wa Mapinduzi katika nidhamu ya Jamhuri ya Kiislamu, Baraza hili baada ya kufanya utafiti wa kina na mpana, na kutumia kipengele cha 108 katika katiba asilia, kwa kufuata wadhifa wa kisheria na kuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu anawaona kwenye maamuzi yao. Leo hii kutokana na rai thabiti, linampitisha Ayatullah Sayyid Mujtaba Hussein Khamenei (Mola amuhifadhi) kuwa ndie Kiongozi mpya wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran.
Mwisho kabisa, tunawashukuru wajumbe wa shura ya muda, na kwa mujibu wa kipengele cha 111 katika katiba asilia, tunawataka wananchi wote, wanazuoni wa Hawza na vyuo vikuu, kumpa kiaga Kiongozi wa Mapinduzi kwa ajili ya kuhifadhi mshikamano, na tunamuomba Mola aendeleze upole na msaada wake katika nchi hii na watu wake.
والسلام عليكم ورحمة الله
Baraza la wataalamu wa uongozi
17/12/1404 - 8/3/2026.
Maoni yako