Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, licha ya uamuzi huo wa kushangaza kutoka Uingereza, waandamanaji waliokuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa “Tumeshinda” na “Mimi si gaidi” walikusanyika nje ya mahakama kwa ajili ya kuyaunga mkono makundi hayo.
Huda Ammori, mmoja wa waanzilishi wa kundi linaloiunga mkono Palestina lijulikanalo kama "Palestine Action", ambaye alikuwa amewasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya hukumu ya mahakama, alisema katika mahojiano: “Lazima niseme kwamba kwa bahati nzuri tulishinda katika mahakama ya rufaa, na Mahakama Kuu iliamua kwamba kupiga marufuku kuiunga mkono Palestina ni kinyume cha sheria kwa sababu kunakiuka uhuru wa kujieleza kwa njia isiyolingana.”
Kutangazwa kwa hukumu hiyo na mahakama ya London pamoja na kuitwa kwa makundi yanayoiunga mkono Palestina kuwa ya kigaidi na serikali — jambo lililoanza kujadiliwa tangu mwaka uliopita — kulikabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka katika mashirika ya kimataifa kama Amnesty International, Jewish Voice for Peace nchini Uingereza, pamoja na mashirika mengine.
Katika mwezi wa Agosti, mamia ya waandamanaji walikamatwa na polisi walipokuwa wamekusanyika mbele ya Bunge la Uingereza huku wakiwa wamebeba mabango ya kuiunga mkono kundi la Palestina.
Chanzo: Time Magazine
Maoni yako