Jumamosi 14 Februari 2026 - 21:30
Ufafanuzi wa ziada kutoka katika Ofisi ya Ayatollah al-Udhma Ja'far Subhani kuhusu hukumu ya kuendesha Pikipiki kwa wanawake

Hawza/ Kufuatia kuchapishwa kwa istiftaa (swali la kifiqhi) kutoka kwa Mtukufu Ayatollah al-Udhma Ja‘far Subhani kuhusu uendeshaji wa baiskeli na pikipiki kwa wanawake, ofisi ya Marjaa huyo imetoa maelezo ya ziada kuhusu mtazamo na rai yake ya kifiqhi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia mawasiliano ya mara kwa mara na ofisi ya Ayatollah al-Uzma Subhani kuhusiana na istiftaa ya tarehe 1404/10/05 H.S, kuhusu uendeshaji wa pikipiki kwa wanawake, ofisi yake imetoa ufafanuzi ufuatao:

Kufuatia kuchapishwa kwa istiftaa ya Mtukufu Ayatollah al-Udhma Ja‘far Subhani kuhusu uendeshaji wa baiskeli na pikipiki kwa wanawake, ofisi ya Marji' huyo imetoa maelezo ya ziada kuhusu mtazamo na rai yake ya kifiqhi.

Kwa mujibu wa mtazamo wa kifiqhi wa Ayatollah al-Udhma Subhani, mhimili wa hukumu ya kisheria si “kitendo chenyewe au chombo chenyewe”, bali ni “anuani” inayojitokeza ndani ya kitendo hicho. Kama ilivyosisitizwa katika jibu la awali kutoka katika ofisi yake kuhusu upandaji farasi kwa wanawake, iwapo upandaji huo utakuwa kwa mavazi yanayobana au kwa namna inayosababisha kuamsha hisia, basi haujuzu. Kwa hiyo, kilicho haramu si upandaji farasi kama chombo maalumu, bali ni kutimia kwa anuani kama vile kujishauwa (tabarruj), kuamsha hisia au kusababisha ufisadi.

Kwa msingi huo, uendeshaji wa pikipiki kwa wanawake hauhesabiwi kuwa haramu kiasili; lakini ikiwa utaambatana na mavazi yasiyofaa au ukasababisha madhara ya kijamii, basi utahukumiwa kuwa haramu. Vinginevyo, uendeshaji wa pikipiki peke yake hauna dalili ya kisheria ya uharamu, na kigezo kikuu ni kuzingatia mizani ya kisheria na maadili katika namna ya kuutekeleza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha