Jumamosi 14 Februari 2026 - 20:30
Mapinduzi ya Kiislamu si kwamba yaliibadilisha Iran pekee, bali eneo lote

Hawza/ Sheikh Khaled al‑Mulla, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlus-Sunna Iraq, huku akisisitiza nafasi ya mabadiliko iliyoletwa na Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alielezea kuwa ni hatua ya kihistoria katika eneo la Mashariki ya Kati, na akaupongeza msimamo wa wananchi wa Iran katika kukabiliana na changamoto.

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Khaled al-Mulla, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlus-Sunna Iraq, katika ujumbe wa video kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, alielezea tukio hilo la kihistoria kuwa ni mabadiliko ya kipekee na ya kimsingi.

Katika ujumbe wake alisema: “22 Bahman inaonesha mabadiliko ambayo watu huru na wenye heshima wa Iran waliyafanya kwa irada thabiti na imani madhubuti kwa Mwenyezi Mungu. Umma huu ulitambua wajibu wake wa Kiungu na ukasimama dhidi ya dikteta wa wakati huo, Shah — ambaye alikuwa wakala wa mfumo wa utawala wa kimataifa wa kiimla na alitumia vibaya utajiri wa nchi yake kwa manufaa ya utawala wa Kizayuni.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Ahlus-Sunna Iraq, huku akirejelea athari za kimataifa za mapinduzi hayo, alisema: 22 Bahman 1357 H.S, ilikuwa siku ambayo haikuibadilisha Iran pekee, bali ilibadilisha eneo lote na kubadilisha sura yake; siku ambayo ilizaa mafunzo na mazingatio makukubwa kama vile muqawama, jihadi, na kusimama pamoja na kadhia ya Palestina.”

Sheikh Khaled al-Mulla alihitimisha kwa kusema: “Katika siku kama hii, tunawapongeza watu wa Iran kwa irada yao ya chuma, na tunathamini uthabiti wao katika miaka mingi dhidi ya mzingiro wa dhuluma, changamoto na vita walivyolazimishwa kuvumilia.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha