Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Alia al-Yasir, mwandishi wa habari katika ulimwengu wa Kiarabu, katika ujumbe wa video kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, aliitaja 22 Bahman kuwa ni tukio linalovuka mipaka ya tarehe ya taifa moja.
Katika ujumbe wake alisema: “22 Bahman si siku ya kawaida, wala si tukio linalohusiana na taifa moja kisha likaisha; bali ni wakati unaofichua namna maamuzi yanavyoundwa na jinsi kila sauti ya upinzani katika ulimwengu huu wenye nguvu hukabiliwa na shinikizo. Ulimwengu unaoweka masharti yake na kumzingira yeyote anayetoka katika utiifu; si kwa sababu ya kosa, bali kwa sababu tu amesema: ‘Sitaki kuwa mfuasi.’”
Mwanahabari huyo, akirejelea msimamo wa Marekani na Israel dhidi ya fikra za Mapinduzi ya Kiislamu, aliongeza kuwa: “Marekani na Israel hazipambani na Iran peke yake, bali zinapambana na fikra; fikra iliyowakera: kwamba nchi ya Kiislamu ihifadhi utambulisho wake na iweze kusema ‘ndiyo’ au ‘hapana’ bila kuomba ruhusa.”
Al-Yasir alisisitiza: “Ndipo 22 Bahman inapokuwa zaidi ya tarehe; ni alama ya ustahimilivu: ustahimilivu wa maisha ya kila siku chini ya shinikizo, ustahimilivu wa uchumi chini ya vikwazo, na ustahimilivu wa maamuzi chini ya vitisho. Somo linalotolewa na wananchi Waislamu wa Iran si maneno ya kinadharia au ya kufikirika, bali ni tajriba halisi kwa Umma wa Kiislamu na watu huru duniani; tajriba inayosema kuwa; utambulisho wa Kiislamu hauhifadhiwi kwa kujichanganya kipofu, haujalindwi kwa ukimya, na hautambuliki kwa kurudi nyuma.”
Mwisho alisema: “Katika ulimwengu uliochafuliwa na utawala wa mabavu na uongo, heshima haiwezi kubaki kwa bahati nasibu, wala Uislamu hauwezi kubaki wenye kuinuka isipokuwa kwa kusimama imara, kwa uthabiti, na kwa kukubali gharama zake.
Shukrani kwa mapinduzi yaliyomrudishia heshima mwanadamu.”
Maoni yako