Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hamas katika taarifa yake iliyotolewa kutokana na mnasaba wa “Siku ya Kutoa Ahadi ya Utii kwa Wanahabari wa Palestina”, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 31 Desemba, ilitangaza kuwa: “Nafasi na mchango wa wanahabari wa Palestina ni wenye nguvu kuliko risasi za wakaliaji, na utaendelea kuwa hivyo.”
Hamas pia ilitoa wito wa hatua ya kimataifa ya pamoja na ya kina, ili viongozi wa utawala wa Israel wawajibishwe kwa sababu ya uhalifu walioutenda dhidi ya wanahabari nchini Palestina.
Hamas ilisema: “Baada ya miaka miwili ya vita na mauaji ya kimbari yaliyojaa umwagaji damu katika Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba 2023 hadi sasa, wanahabari na waandishi wa habari 257 wameuawa kwa mikono ya utawala wa Israel.”
Harakati hiyo iliongeza: “Vita vya Ghaza vimeondoa pazia la utawala haramu wa Israel na kuufichua kama adui hatari zaidi na mkuu wa kusambazwa kwa ukweli na taaluma ya uandishi wa habari, taaluma ambayo inawakilisha sauti na taswira ya waliodhulumiwa. Wanahabari, kwa kuripoti matukio halisi katika ardhi hii kwenye ulimwengu unaowazunguka—licha ya kulengwa kwao mara kwa mara na moja kwa moja—wamesaidia kuyabadilisha matangazo ya propaganda ya utawala huu wa kinyama, na kufichua ukweli wake mchafu.”
Chanzo: Kituo cha Habari cha Palestina.
Maoni yako