Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ali al-Khatib, Makamu Rais wa Baraza Kuu la Mashia, katika kumkaribisha Papa alisema: Tunakukaribisha na tunakushukuru kwa misimamo yako dhidi ya dhulma katika kipindi hiki kigumu ambacho nchi yetu inapitia.
Sheikh Abdul Latif Daryan alisisitiza dhamira ya Lebanon juu ya umoja wa kitaifa, uhuru wa dini na haki za binadamu katika nchi hiyo, na kusema: Sisi nchini Lebanon tunasisitiza sana juu ya msimamo wa kitaifa. Tunaheshimu haki za binadamu na hatuingilii wala kushambulia masuala ya nchi nyingine.
Askofu wa Kanisa la Othodoksi, “John wa Kumi,” naye pia alimkaribisha Papa na kuongeza: Karibu Lebanon, nchi ya kipekee ambayo Ukristo na Uislamu vimeungana na kushikana kwa karibu.
Leo wa Kumi na Nne aliwahutubia watu wa Lebanon kwa ujumbe wa matumaini na subira, na akaupongeza ustahimilivu wao katikati ya changamoto zinazoendelea. Papa katika hotuba yake kutoka Ikulu ya Baabda alisema: “Kwetu sisi ni furaha kubwa kuitembelea ardhi hii, mahali ambapo amani ni zaidi ya neno moja — ni tamanio, ni wito, ni zawadi na ni karakana iliyo wazi daima.”
Chanzo: Al-Manar
Maoni yako