Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, tangazo hili la Ireland limekuja kufuatia maombi na hatua kama hizo zilizowasilishwa na marais wa vyama vya soka vya Norway na Uturuki. Chanzo kimoja cha kuaminika ambacho hakikutaka kutajwa jina lake kiliiambia shirika la Reuters kwamba UEFA ilikuwa imepanga kupiga kura rasmi mwanzoni mwa mwezi uliopita kuhusu kusimamishwa kwa Israel.
Hatua hii imechukuliwa baada ya mara kadhaa wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuziomba FIFA na UEFA kuisimamisha Israel kushiriki katika soka la kimataifa, kwa mujibu wa ripoti ya tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliyotaja kuwa Israel imefanya mauaji ya kimbari wakati wa vita vya Ghaza na kutenda uhalifu mbaya zaidi dhidi ya ubinadamu katika eneo hilo dogo.
Vyanzo kadhaa vimeeleza kuwa kutofanyika kwa upigaji kura rasmi kulisababishwa na msimamo na vitisho vya Marekani ambayo ni miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa utawala wa Kizayuni, kwani nchi hiyo ni mmoja wa wenyeji wenza wa Kombe la Dunia lijalo.
Ireland imekuwa miongoni mwa wakosoaji wakubwa ndani ya Umoja wa Ulaya tangia kuanza kwa vita vya Israel huko Ghaza.
Chanzo: Reuters
Maoni yako