Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, vitu 44 vya kihistoria na vya kale vilivyogunduliwa Ghaza vinahifadhiwa katika Makumbusho ya Geneva, Uswisi. Miongoni mwa vitu hivyo ni mitungi ya udongo, sanamu, vyungu na taa za mafuta. Vitu hivyo vinaoneshwa katika sehemu maalumu ya makumbusho iitwayo Urithi Ulio Hatarini.
Beatrice Blandin, msimamizi wa sehemu hiyo katika makumbusho katika mahojiano alisema kwamba: “Vtu hivi ni sehemu ya historia na roho ya Ghaza, na vinaakisi historia halisi ya watu waliokuwa wakiishi huko tangia zamani.” Aliongeza kuwa mkusanyo wa Ghaza una jumla ya vipande 530 vinavyohifadhiwa katika masanduku na ghala salama huko Geneva, na kutokana na uharibifu na uhalifu wa utawala wa Kizayuni huko Ghaza, kwa sasa hakuna uwezekano wa kurejeshwa Ghaza.
Mmoja wa wajumbe wa Baraza la Jiji la Geneva alisisitiza umuhimu wa kulinda na kutunza athari hizo, akisema kuwa “vikundi vyenye fikra mgando daima huwa na azma ya kuharibu urithi wa kihistoria na wa ustaarabu.”
Chanzo: Al-Monitor.
Maoni yako