Jumatatu 10 Novemba 2025 - 21:10
Darul-Ilm ya Bangkok Yawa Mwenyeji wa Waombolezaji wa Bibi Fatima (a.s.)

Hawza/ Kutokana na mnasaba wa siku za kumbukumbu ya shahada ya Bibi mkubwa wa Uislamu, Bibi Fatima Zahra (amani ya Mungu iwe juu yake), hafla maalumu iliandaliwa katika Darul-Ilm mjini Bangkok, kwa ushiriki wa kundi la wanazuoni, wanafunzi wa vyuo, wanafunzi wa dini, Waislamu wa Thailand, na wapenda mafundisho ya Ahlul-Bayt (as).

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla hiyo ilijumuisha hotuba ya Hujjatul-Islam Sayyid Saeed Khalkhali, aliyezungumzia kuhusiana na mwenendo wa maisha binafsi wa Bibi Fatima (a.s.) na umuhimu wa kushiriki katika masuala ya kijamii.

Katika maelezo yake, alibainisha nafasi ya kipekee ya Bibi Fatima (a.s.) katika mfumo wa Ahlul-Bayt (a.s.) akisema: “Kumjua Fatima Zahra (a.s.) ni kumjua mwanadamu mkamilifu. Yeye hakuwa tu binti wa Mtume (s.a.w.w) na mke wa Imam Ali (a.s.), bali alikuwa taswira halisi ya imani, uchamungu, elimu, na uwajibikaji mbele ya Mwenyezi Mungu na jamii.”

Chanzo: Idara ya Mahusiano ya Umma na Habari ya Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha