Jumamosi 18 Oktoba 2025 - 16:13
Uvamizi wa Israel dhidi ya Lebanon hautabadilisha kwa vyovyote mlingano wa ustahimilivu

Hawza/ Hasan ‘Izzuddin amesema kuwa: Adui wa Kizayuni katika siku za hivi karibuni amezisha mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, kwa kuwa anaamini kwamba kupitia shinikizo la kisiasa na kiuchumi, na kwa kulenga maslahi ya wananchi, anaweza kuwazuia wakazi kurejea katika vijiji vyao vya mpakani.

Kwa mujibu wa idara ya tarajama ya Shirika la Habari la Hawza, Hasan ‘Izzuddin, mjumbe wa kikundi cha wabunge wa Uaminifu kwa Muqawama na mbunge wa Lebanon, alihutubu katika hafla iliyofanywa na Hizbullah kutokana na kumbukumbu ya shahidi Abbas Muhammad Salameh katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangia kuuawa kwake kishahidi.

Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Imam al-Mujtaba (a.s.) kilichopo katika eneo la al-San Tirez, na ilihudhuriwa na Husein Fadlallah, mkuu wa eneo la Beirut wa Hizbullah, pamoja na kundi la wanazuoni, waheshimiwa, familia za mashahidi na wakazi wa eneo hilo.

Hasan ‘Izzuddin katika hotuba yake alisema: “Adui wa Kizayuni katika siku za hivi karibuni ameongeza mashambulizi yake dhidi ya Lebanon kwa sababu anaamini kuwa, kupitia shinikizo la kisiasa na kiuchumi na kwa kulenga maslahi ya wananchi anaweza kuwazuia wakazi kurejea katika vijiji vyao vya mpakani, na hivyo, kwa dhana yake, kufikia moja ya malengo yake — yaani kuzuia ujenzi na ukarabati. Hata hivyo, jambo hili kwa vyovyote vile halitabadilisha ulingano wa ustahimilivu.

Akaongeza kusema: “Tumeona kwamba serikali, baada ya uvamizi wa mji wa Msaylih, kinyume na yaliyokuwa yakitokea huko nyuma, imebadilisha msimamo wake kidogo, kwa sababu Wizara ya Mambo ya Nje ilitoa tamko la kulaani uvamizi huo. Hapo awali, kwa masikitiko, wizara hiyo ilikuwa ikionekana kana kwamba iko nje ya muktadha wa mshikamano wa kitaifa na inalenga maslahi finyu ya kichama. Pia tulishuhudia mawaziri wakitembelea eneo lililovamiwa na kukagua hasara iliyosababishwa na uvamizi huo.”

‘Azzuddin akaendelea kusema: “Waziri Mkuu pia alitaka kuwasilishwa malalamiko kwenye Baraza la Usalama, jambo ambalo ni chanya, lakini halitoshi kabisa. Serikali ina wajibu wa kulinda wananchi na taifa lake, na kuchukua hatua zitakazozuia kuendelea kwa uvamizi, mauaji, uhalifu wa adui huyu na ukiukaji wa mamlaka ya nchi.”

Mjumbe huyo alimtaka Waziri Mkuu kuanza juhudi za kujenga upya nchi, na akasema: “Masuala haya yote ni miongoni mwa vipaumbele vya msingi ambavyo serikali hii inapaswa kuyatekeleza, na inaweza kutumia diplomasia yake pamoja na marafiki wa Lebanon na washirika wa kimataifa na wa kieneo ili kuwekea adui shinikizo.”

Akasema kwa kusisitiza: “Muqawama utaendelea kwa nguvu na kwa taathira, kwa sababu ni urithi wa jihadi, kujitolea na kujitoa mhanga kizazi baada ya kizazi. Tukio la mwisho katika urithi huo wa kizazi ni lile lililotokea katika uwanja wa michezo wakati wa hafla kubwa ya skauti ‘Vizazi vya Sayyid’, lililofanyika katika hitimisho la maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi Sayyid Hasan Nasrullah na Sayyid Hashim Safi al-Din.”

‘Azzuddin akasema: “Sisi ni waaminifu wa damu safi za mashahidi, ambazo kupitia hizo tunachora taswira ya nchi yetu tukufu ya Lebanon — nchi ambayo mashahidi hawa walitaka iwe na serikali yenye nguvu, yenye uwezo na uadilifu, inayokuza hisia za uwiano na uaminifu wa wananchi kwake.”

Mbunge huyo wa Lebanon alisisitiza: “Mashahidi na wapiganaji katika vita vya ‘Awali ya Ushujaa’ waliweza, kwa ustahimilivu wao, kuzuia uvamizi wa adui dhidi ya Lebanon na kuzuia ardhi ya Lebanon isikaliwe. Walishinda malengo ya adui, hasa jaribio lake la kuigeuza Lebanon kuwa koloni la Israeli au kuwa himaya ya Marekani. Walimzuia adui asiweze kukalia, kudhibiti au kutawala, licha ya kuwa alituma takribani aina tano za kijeshi katika mapambano hayo.”

Mjumbe wa kikundi cha wabunge wa Muqawama alibainisha pia: “Lebanon itaendelea kujivunia uhusiano wake wa Kiarabu na utambulisho wake wa kimuqawama. Uwezo wake wa kujilinda, kulinda wananchi wake na rasilimali zake, kwa ajili ya kuhifadhi mamlaka ya kitaifa, uhuru wa maamuzi, na kuendeleza nafasi, heshima na utu wa Lebanon, utabaki imara.”

Akamalizia kwa kusema: “Licha ya kelele zote na kampeni za upotoshaji zinazoendelea — hasa yale tuliyoyaona huko Sharm al-Sheikh na katika Bunge la Israel, pamoja na kiburi na jeuri aliyoionesha Trump kwa waliokuwepo katika kikao hicho — silaha ya kitaifa na huru ya Muqawama itaendelea kubaki kwa ajili ya kulinda na kuitetea Lebanon.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha