Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Makarim Shirazi alipokutana na wanafunzi wa dini, walimu, wasimamizi na wafanyakazi wa vituo vilivyo chini ya usimamizi wake, akiirejea hadithi kutoka kwa Imam Hasan al-Askari (a.s) ambaye amesema:
«خَیرُ الأُمورِ اثنان: الإیمانُ بالله و البِرُّ بالإخوان»“Mambo mawili ndiyo bora zaidi: kumuamini Mwenyezi Mungu na kuwafanyia wema ndugu”.
Alieleza kuwa hadithi hii inaonyesha kwamba kumuamini Mwenyezi Mungu kuwatendea wema ndugu wa kidini ni nguzo mbili kuu katika njia ya kheri na wema.
Siri ya mafanikio ya wanazuoni kwa mtazamo wa Marja‘
Mwanachuoni mkubwa huyu alibainisha kwamba siri ya mafanikio ya wanazuoni wa dini inahusiana na mambo kadhaa, akiongeza kuwa: nidhamu na juhudi za kudumu, usafi wa nia, na heshima kwa wakubwa wa dini ni nguzo kuu katika maendeleo ya mwanafunzi wa dini. Mwanadamu hapaswi kuchoka katika njia ya elimu, bali aifanye nia yake iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na awaheshimu walimu na wanazuoni wa dini.
Mtukufu Ayatullah Makarim Shirazi, akiirejea historia ya hawza, alifafanua kuwa Sheikh Tusi, licha ya shinikizo na uhasama wa maadui huko Baghdad, hakukata tamaa, bali alihama kwenda Najaf na kuanzisha hawza ambayo kwa kipindi cha miaka elfu moja imeendelea kuangaza taa ya elimu na fiqhi. Haya ni matunda ya subira, juhudi na imani.
“Bado ninaendelea na shughuli za kielimu”
Alibainisha kuwa yeye bado anaendelea kikamilifu na shughuli za kielimu:
“Tunaendelea na kazi ya kusahihisha mkusanyiko wa ‘Bihar al-Anwar’ hadi juzuu ya tisini na sita (96). Pia ninaendelea kufundisha masomo ya hawza mara tatu kwa wiki.”
Tuzo ya uandishi wa “Tafsiri Amthali”
Aidha, alikumbusha tajiriba ya kuandika “Tafsiri ya Amthal”, akisema:
“Wakati ilipohisiwa uhitaji wa tafsiri ya Qur’ani kwa lugha ya Kiajemi na ya kisasa, kwa msaada wa wanavyuoni vijana wenye vipaji, uandishi wa Tafsiri Amthali ulianza. Leo hii, kazi hii imetafsiriwa kwa lugha mbalimbali ikiwemo Kiarabu, Kiurdu, Kituruki, Kiingereza na Kihausa. Baada ya hapo, maelezo ya Nahjul-Balagha na Sahifa Sajjadiyya pia yaliandaliwa na kupokelewa kwa mapokezi makubwa.”
Msisitizo wa kutumia akili bandia na teknolojia za kisasa ndani ya hawza
Mtukufu Ayatullah Makarim Shirazi alieleza kwamba teknolojia za kisasa zina nafasi muhimu katika maendeleo ya elimu, akasisitiza:
“Hawza zinapaswa kutumia zana za kisasa kama vile akili bandia (AI). Kama vile baadhi ya watu katika zama zilizopita walivyopinga vipaza sauti na simu, ndivyo ambavyo leo hatupaswi kusimama dhidi ya teknolojia mpya. Badala yake, tunapaswa kuwa wa kwanza kuitumia teknolojia hiyo katika njia ya kueneza dini.”
Nasaha muhimu na zenye manufaa
Mwisho wa hotuba, Mheshimiwa Ayatullah Makarim Shirazi akiwahutubia wanafunzi na walimu wa hawza alisema:
“Kwa imani, juhudi na ikhlasi yenu, na kwa kutumia zana za kisasa, jazeni mapengo ya kielimu na kiutamaduni. Msiache dua, kwani dua ina athari. Mimi daima katika qunut za Swala zangu nawamuombea mafanikio wanavyuoni na wanafunzi wa hawza, na nawaomba pia mniombee dua.”
Ushiriki wa viongozi wa hawza katika kikao hicho walihudhuria pia:
Ayatullah Muhammad Mahdi Shabzindadar, Katibu wa Baraza Kuu la Hawza;
Ayatullah Alireza A‘rafi, Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu nchini Iran;
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Maliki, Naibu Mkurugenzi wa Hawza ya Qom Iran;
pamoja na baadhi ya viongozi na wasomi wengine wa kielimu.
Mwisho wa taarifa.
Maoni yako