Jumatatu 6 Oktoba 2025 - 15:45
Kukandamizwa kwa Sauti za Wanaotetea Haki Kumeufichua Uso wa Kweli wa Utawala wa Kizayuni

Hawza/ Thaqalain Ali Jafari, katika taarifa yake iliyo laani vikali shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya “Flotilla ya Kimataifa ya Ṣumūd‌”, alisisitiza kuwa mwenendo wa Israel dhidi ya wanaharakati wa amani unaonesha uso wa kweli wa utawala huu na uadui wake wa wazi dhidi ya ubinadamu. Alitoa wito kwa taasisi za kimataifa kuchukua hatua za haraka kuwaachia waliokamatwa na kuunga mkono taifa dhulumiwa la Palestina.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Thaqalain Ali Jafari, Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Asghariyya Pakistan, katika taarifa rasmi alilitaja shambulio la majeshi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya msafara wa “Flotilla ya Kimataifa ya Ṣumūd‌” na kukamatwa kwa watu mashuhuri wa kimataifa akiwemo Seneta Mushtaq Ahmad na wenzake kuwa ni jinai ya wazi dhidi ya ubinadamu.

Alisisitiza kuwa: “Kitendo hiki kinaonesha uhalisia wa kiburi na uovu wa kibinadamu wa utawala wa Kizayuni na wafuasi wake, ambao hata misaada ya kibinadamu kwa watu wanyonge wa Ghaza wanaogopa kufikishwa.”

Thaqalain Jafari akirejea ukandamizaji wa wanaharakati wa amani na utawala wa Kizayuni aliongeza: “Israel na wafuasi wake, kwa kukandamiza sauti za wanaotetea haki, wamefichua wazi wazi uso wao wa kweli na wa kupinga ubinadamu mbele ya dunia nzima. Wale wanaojitokeza kuwatetea Wapalestina na kufikisha ujumbe wa haki na uadilifu, ndio mashujaa wa kweli wa ubinadamu, na majina yao pamoja na kujitolea kwao yataendelea kukumbukwa katika historia.”

Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Asghariyya Pakistan mwishoni aliutaka Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa zinazotetea haki za binadamu kulaani jinai hizi, kuchukua hatua za haraka kuwaachia waliokamatwa, na kuchukua nafasi madhubuti na ya kivitendo katika kuunga mkono haki ya uhuru na kujitawala kwa taifa la Palestina.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha