Jumatatu 29 Septemba 2025 - 09:26
Shahada ya Sayyid Hassan Nasrullah imefungua ukurasa mpya wa kuunga mkono jukwaa la mapambano

Hawzah / Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrallah, amesema: Damu safi ya shahidi huyu mpiganaji haikusababisha kudhoofika kwa jukwaa la mapambano, bali ilisababisha wimbi jipya la uungaji mkono, ustahimilivu na mwamko wa Kiislamu kote katika eneo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Nasrallah na mashahidi wenzake, Sayyid Sajid Ali Naqvi — Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan — katika ujumbe wake huku akitoa heshima kwa nafasi ya juu ya mashahidi hao, amesisitiza juu ya nafasi ya kihistoria yao katika kuimarisha jukwaa la mapambano.

Akitukuza shakhsia na juhudi za shahidi Nasrullah, amesema: Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah alikuwa miongoni mwa wapiganaji mashuhuri wa zama zetu; uhai wake ulikuwa chanzo cha msukumo na ushahidi wake ilikuwa nukta muhimu katika historia ya mapambano. Kupata shahada kwake kuliongeza uungaji mkono wa wananchi kwa Hizbullah, na harakati ya ukombozi wa Quds Tukufu pamoja na vuguvugu la mapambano ya Kiislamu katika eneo lote ilipata uhai mpya; kiasi kwamba nguvu za ubeberu zilijikuta zikikumbwa na fedheha, udhalili na kushindwa mara kwa mara.

Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Kipalestina akielezea nafasi ya kimataifa ya mashahidi wa mapambano, ameongeza: Ushahidi wa viongozi hawa haukuathiri tu eneo, bali hata katika kiwango cha kimataifa ulileta mabadiliko makubwa. Kujitolea huku kuliufanya uso halisi wa uistikbari uonekane zaidi na kuimarisha azma ya mataifa kusimama dhidi ya uvamizi na ubeberu.

Akiendelea akizungumzia hali ya sasa ya eneo, amesema: Ukweli ni kwamba mizizi ya jinai zote hizi ni ubeberu wa kimataifa. Utawala wa Kizayuni unasaidiwa na nguvu za kibeberu; kuanzia ufadhili na silaha, hadi teknolojia za kisasa, taarifa na mipango yote — yote hufanyika chini ya usimamizi wa ukoloni. Ndiyo maana utawala huu umejipa ruhusa ya kuishushia Ghaza mateso ya zaidi ya miaka miwili na hata kuiteketeza Lebanon kwa moto wa vita. Katika hali hii, ni jukumu la jumuiya ya kimataifa kusitisha ukatili na unyama huu.

Hujjatul-Islam Sayyid Sajid Naqvi katika sehemu nyingine ya maneno yake ametaja nafasi muhimu ya Pakistan na kusema: Pakistan ina uwezo na ushawishi mkubwa. Ikiwa taasisi yetu ya diplomasia itaingia uwanjani kwa nguvu zote na kuunda mitandao mikali ya kushawishi, ikiongeza shinikizo la kimataifa dhidi ya ubeberu, inaweza kusaidia kukomesha jinai huko Ghaza, Palestina na Lebanon, na hata kuzuia kutokea kwa vita vikuu vya tatu vya dunia.

Aidha, amesisitiza juu ya haja ya kuimarisha juhudi za kibinadamu: Leo hii, ni lazima misaada kwa watu wanaodhulumiwa wa Ghaza, Palestina na Lebanon iongezwe na iendelee katika kiwango kikubwa zaidi na chenye ufanisi.

Mwisho, Hujjatul-Islam Sayyid Sajid Ali Naqvi huku akitoa heshima kwa nafasi tukufu ya shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na mashahidi wenzake, amesisitiza: Wapiganaji hawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa kujitolea kwao sana wamekuwa kielelezo cha milele kwa Umma wa Kiislamu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi hawa wapendwa na awape Hizbullah tawfiki na ustahimilivu ili waendeleze njia yao tukufu kwa nguvu na ushindi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha